Mazao ya Alizeti yakiwa yamestawi na kunawili kwenye shamba la wakulima wakubwa wa Halmashauri ya wilaya ya Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge [Kushoto] Akionyesha mfano wa mbegu bora ya alizeti iliyopandwa na wakulima , akiwa ameambatana na Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili [kulia].
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Singida Nathalia Moshi Akisoma taarifa ya hali uzalishaji wa zao la Alizeti kwenye Halmashauri hiyo baada ya zaira ya mkuu wa mkoa wa Singida Kutembelea Mashamba ya wakulima.Jitihada hizo pamoja na mambo
mengine zinakwenda kupunguza gharama kubwa ya takribani Bilioni 500 ambazo serikali
hulazimika kila mwaka kutumia kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.
Kwa mujibu wa Takwimu za Mkoa mpaka
sasa tayari ekari 239,700 za alizeti zimelimwa na kupandwa aina tofauti za mbegu
za zao hilo zipatazo tani 469.
Hata hivyo akiwa kwenye ziara ya
kutembelea mashamba mbalimbali ya alizeti yaliyopo Halmashauri ya Wilaya ya
Singida Mkoani hapa jana , Mkuu wa mkoa Dkt.
Binilith Mahenge aliagiza kuitishwa kwa kikao cha Wadau wa mnyororo wa zao hilo
ili kwa pamoja kujadili namna nzuri ya kuhakikisha kunakuwa na bei nzuri ambayo
itawanufaisha wakulima wote wa zao la alizeti.
“Tunategemea
kuvuna mara mbili zaidi ya mwaka jana mavuno yatakuwa makubwa kwahiyo chakukubaliana hapa tuandae
kikao cha wadau waliotoa mbegu, wale waliolima na wenye viwanda ili tuangalie nani atachukua tani ngapi na kwa bei
ipi, isitokee wananchi wakaanza kuangaika
mtu akawa anachukua Mazao kwa bei ya chini” Alisema Dkt. Mahenge.
Dkt. Mahenge alisema kupitia vikao vya
mkoa kuhusu mkakati wa kilimo cha alizeti zilianishwa ekari zitakazozalishwa kwa mkoa wa
Singida na ukafanyika mgawanyo kwa kila halmashauri ambapo serikali
ilitoa ruzuku ya mbegu kwa wakulima jambo ambalo
limeongeza uzalishaji akitolea
mfano Halmashauri ya Wilaya ya Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida Akipewa Maelezo ya mashamba ya alizeti kwenye ziara hiyo.
Akiwa Kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Pasikasi Muragili alisema ikiwa mwenendo wa kilimo cha zao hilo utaendelea vizuri mkoa huo utachangia kiwango kikubwa kwenye uzalishaji wa mafuta hapa nchini kupitia mazao ambayo yamelimwa na wakulima.
Mhandisi Muragili alisema pamoja na
kutofikia malengo ya serikali ya kupata
mbegu walizoomba lakini wakulima walitafuta mbegu
kutoka kwa wadau wengine hivyo kwa kiwango cha mbegu walizopanda wakulima hao kupata mavuno mengi na kuisaidia kuongeza uzalisha mafuta yakutosha.
Akiwasilisha taarifa ya uzalishaji
wa Alizeti katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida Afisa Kilimo Bi Nathalia
Moshi amesema katika msimu wa kilimo
2021/22 ilitarajia hecta 38,936 na
kuvuta tani 73,936 ambapo halmashauri hiyo iliomba mbegu tani 195 kutoka kwa wakala wa mbegu Asa lakini mpaka sasa
wamepata mbegu tani 76.01 ambazo
zimesambazwa katika kata 21 .
Nathalia aliongeza kuwa Halmashauri
imeshirikiana na wadau mbalimbali wakiweo Mradi wa kukabiliana na Madhara ya
Ukivo 19 unaofadhiliwa na mfuko wa kimataifa wa
maendeleo ya kilimo IFAD ,Mwenge
Sunflower , pyxus , Mount Meru Millers
limited kuwapatia wakulima mbegu za
alizeti.
Mbegu Bora ya Alizeti ikiwa yamestawi Shambani
0 comments:
Post a Comment