Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) Mhandisi Deogratius Kamala akimtwisha Ndoo ya maji Mkazi wa Mwankoko, Manispaa ya Singida Remister Mkhotia ikiwa ni moja huduma inayotolewa kwa sasa na mamlaka hiyo kwa kutumia teknolojia ya utoaji maji kupitia Magati kwa mfumo wa e-water wakati wa uzinduzi wa wiki ya maji kwa mkoani Singida.
1. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Suwasa Hosea Maghimbi
akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Bodi
ya SUWASA Mhandisi Deogratius Kamala wa namna ya uendeshaji mitambo iliyopo
kwenye chanzo cha maji cha Mamlaka hiyo
kilichopo eneo la Mwankoko.
1.
Diwani wa kata ya Mandewa Baraka Hamis
akizungumza kwenye uzinduzi huo.
KATIKA kuadhimisha wiki ya Maji Mamlaka
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imewataka wananchi wote
mkoani hapa kuhakikisha wanaendelea kutunza vyanzo vyote vya maji vilivyopo
sambamba na kufichua taarifa za kihalifu dhidi ya yeyote mwenye nia ovu ya kuhujumu
miundombinu ya rasilimali za maji kwa ustawi endelevu wa rasilimali hiyo muhimu
isiyo na mbadala wake.
Aidha, kupitia maadhimisho hayo
yenye kauli mbiu isemayo; ‘Maji chini ya Ardhi Hazina
Isiyoonekana kwa Maendeleo Endelevu,’
Suwasa imesisitiza umuhimu wa watumia huduma hiyo kulipa Ankara za maji kwa
wakati sanjari na kuwataka wote wenye malimbikizo ya madeni kufika katika ofisi
hizo kwa lengo la kuingia mikataba maalumu na mamlaka hiyo ili kuweza kulipa
bili husika ndani ya wakati.
Akizungumza katika uzinduzi wa wiki
ya maji mkoani hapa iliyoshirikisha SUWASA, Wakala wa Maji na Usafi wa
Mazingira Vijijini (RUWASA), Chuo cha Maji Tawi la Singida, Bonde la Kati na Maabara
za Ubora wa Maji, Mwenyekiti wa Bodi ya Suwasa Mhandisi Deogratius Kamala
alisema maadhimisho ya mwaka huu ni mahsusi kwa ajili ya utoaji elimu, kueleza
kwa umma miradi inayotekelezwa sanjari na kupokea maoni kutoka kwa watumia
huduma za maji
“Maadhimisho
ya mwaka huu yanafanyika nchini kote tangu Machi 16 mpaka kilele chake ifikapo
Machi 22 ikiwa ni kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1946,” alisema Mhandisi Kamala
1. Kaimu Meneja wa ufundi wa Suwasa Mhandisi Elisha
Kivuyo akitoa maalezo ya kitaalamu kwenye eneo la matenki ya kuhifadhi na
kutibu maji yaliyopo eneo la Mandewa
Hata hivyo, alisisitiza jamii kuendelea kuenzi, kutunza, kulinda na kuheshimu vyanzo vya maji vilivyopo ili kwa pamoja na umoja kuwezesha jamii na mamlaka za maji zilizopo ili kuifanya rasilimali hiyo kuwa endelevu kwa vizazi vya sasa na baadaye.
1 Baadhi ya Maafisa wa maji wakifuatilia uzinduzi wa wiki ya
maji.
1. Baadhi ya Vifaa vya kisasa vya kutoa huduma za
kuhifadhi na kutibu maji yanayotoka kwenye chanzo cha maji Mwankoko.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Suwasa Hosea Maghimbi alisema mamlaka hiyo kwa kiasi kikubwa inategemea ushirikiano wa jamii hususani kwenye eneo la kunyanyua mapato katika kuiwezesha kufanikisha azma yake chanya ya kuendelea kusogeza karibu huduma zake kwa tija na ufanisi.
Kaimu Meneja wa ufundi wa Suwasa Mhandisi
Elisha Kivuyo aliitaja baadhi
ya miradi inayotekelezwa na mamlaka hiyo
kuwa ni pamoja na ujenzi wa tanki
la maji lenye ujazo wa kutunza maji mita
cubic 200 pamoja na pampu za kuwezesha
kusukuma maji hadi eneo la Somoku ,
Aidha mradi mwingine ni ujenzi wa
kisima eneo la Unyambwa ambao umekamilika na hatua inayofuata ni uwekaji wa
miundombinu ya umeme na pampu za kusukuma maji lengo ni kuhakikisha eneo lote
la manispaa linakuwa na huduma za maji
za uhakika.
“Nitoe
rai kwa wananchi kuchangamkia ofa ya kuunganishiwa maji kwa gharama ya shilingi
laki moja pekee kwa wakazi wote wanaoishi kuzunguka eneo la mradi, lakini pia
wafike ofisi za Suwasa ili kujipatia huduma zingine zinazoendelea kutolewa kupitia
miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa fedha za Uviko”
Katika hafla ya uzinduzi huo wadau
mbalimbali wa maji na wananchi wakiongozwa
na Diwani wa Kata ya Mandewa Baraka
Hamis walipata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na suwasa
ndani ya manispaa mkoani hapa, ikiwemo chanzo cha maji Mwankoko, Matanki makubwa ya kuhifadhi maji eneo la mandewa na kuangalia moja ya teknolojia ya mfumo wa
utoaji wa maji kupitia
Magati kwa mfumo wa e-water.
Kupitia Mfumo huo, ikilinganishwa na kipindi cha nyuma kwa sasa
kuna mabadiliko makubwa kutokana
wananchi wenyewe kujipatia huduma ya
maji bila ya uwepo wa wakala kama
ilivyokuwa hapo awali.
Mkazi wa Mwankoko Remister Mkhotia akipata huduma ya maji kupitia teknolojia ya E-water
1. Afisa uhusiano wa SUWASA James Malima
akizungumza na wananchi wa Mwankoko kwenye tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment