Dkt Nangi William Mratibu wa kifua kikuu na ukoma Mkoani Mwanza
Dkt Clement Morabu kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mganga Mkuu Hospitali ya Wilaya ya Misungwi
wananchi
Mgeni rasmi akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa afya
Na Maganga James Gwensaga - Mwanza
Katika kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa kifua
kikuu mkoa wa Mwanza umefanikiwa kwa kiwango kikubwa kupitia Mikakati mbalimbali iliyoiweka ikiwemo kuanzishwa kwa wilaya za kimkakati za kifua kikuu zipatazo
tisa za Buchosa , Kwimba , Magu,
Misungwi, Mwanza East, Mwanza North, Mwanza south, Sengerema na Ukerewe kwa
lengo la kuibua wagonjwa 4745 ili kufikia asilimia moja ya lengo la Mkoa.
Mafanikio mengine ni
kila Wilaya ya kifua kikuu kuwa na mratibu wa kifua kikuu ambaye
atashirikiana na Mratibu wa Kifua kikuu na Ukimwi, uwepo wa Muuguzi wa kutoa
dawa za kifua kikuu (DOT Nurse) kila kituo cha tiba, ongezeko la vituo vya
kupimia kifua kikuu 88 pamoja na uwepo wa gari maalumu la kliniki Tembezi ya
kifua kikuu, gari ambalo linatoa huduma Kanda ya Ziwa.
Hayo yameelezwa na Dkt Nangi William Mratibu wa
kifua kikuu na ukoma Mkoani Mwanza, March
24, 2022 wakati akitoa taarifa ya hali ya kifua kikuu Mkoani Mwanza kwa Mgeni Rasmi Dkt Clement Morabu kaimu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mganga Mkuu Hospitali ya Wilaya ya
Misungwi kwenye maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu nchini ambayo kiMkoa
yaliyofanyika Wilayani Misungwi.
“ Leo March 24, 2022 tunaadhimisha siku ya kifua
kikuu Duniani ikiwa ni kumbukumbu ya matokeo makubwa ya ugunduzi wa vimelea
vinavyosababisha ugonjwa wa kifua kikuu vinavyojulikana kwa jina la Mycobacterium
tuberculosis ambapo mtafiti na Mwana Mikrobailojia Daktari Robert Koch
aliitangazia dunia matokeo ya utafiti wake katika Jiji la Berlin mwaka 1882.”
Alisema Dkt Nangi
Aidha aliyataja mafaniko mengine ni uwepo wa vituo 275 vya kutolea dawa za kifua kikuu,
mashine za x-ray 17 ambazo pamoja na kupima magonjwa mengine hutumika pia
kupima kifua kikuu pamoja na uwepo wa kituo maalum cha huduma za wagonjwa wa
kifua kikuu sugu(MDR-TB) Kilichopo Bugando.
Alisema hadi
kufikia Disemba 2021, Mkoa wa Mwanza ulikuwa na jumla ya wagonjwa wa
kifua kikuu 4409 na wenye kifua kikuu sugu 17 huku katiki yao waliopima vvu ni
4248 na waliopatikana na maambukizi ni 991.
Aidha aliwapongeza wadau wa maendeleo katika
seksheni ya Afya ambao ni Amref anayetekeleza mradi wa afya shirikishi kwa
ushirikiano na shirika la SHDEPHA+ Kahama katika kutoa huduma za kifua kikuu
katika ngazi ya Jamii ambapo katika mradi huo wahudumu wapatao 99 pamoja na
waendesha bopdaboda hukusanya sampuli na kusafirisha kwenye vituo vya upimaji.
“ Pia tunashukuru shirika la ICAP kupitia mradi wao
wa FIKIA+ pia kwa kushirikiana na
shirika la SHDEPHA + la Kahama anayetekeleza huduma za kifua kikuu na Ukimwi
ngazi ya Jamii.
Alizitaja changamoto mbalimbali zinazaowakabili
katika utekelezaji wa mapambano dhidi ya kifua kikuu kuwa ni uhaba wa mara kwa mara wa upatikanaji wa makopo ya kukusanyia
sampuli za makohozi pamoja na kuharibika mara kwa mara kwa mashine za Gene
x-pert hali inayorudisha nyuma jitihada za kuibua wagonjwa wa kifua kikuu.
Kwa upande wake Dkt Clement Morabu kaimu Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza na Mganga Mkuu Hospitali ya Wilaya ya Misungwi amefurahishwa
sana kwa namna ya mkoa ulivyojipanga katika mapambano ya kifua kikuu.
“ Niwapongeze sana Mkoa wa Mwanza kupitia taarifa ya
mratibu ikiwemo kuanzisha wilaya za kimkakati katika kukabiliana na ugonjwa huu
na nimefurahi sana kuona hata kwenye maadhimisho haya kuna banda la uchunguzi
wa kifua kikuu haya ni mafanikio makubwa sana hongereni.” Alisema Dkt Clement
Kitaifa Siku ya Kifua kikuu Duniani uadhimishwa kila tarehe 24 mwezi Machi na kwa mwaka huu, iliadhimishwa Kitaifa Mkoani Tanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu Waziri wa Afya na Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni OKOA MAISHA, WEKEZA KATIKA KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU NCHINI.
0 comments:
Post a Comment