METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, January 21, 2022

TUME HURU YA UCHAGUZI LESOTHO YAMTEMBELEA MZEE PINDA SHAMBANI KWAKE

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda (kulia) akizungumza na ugeni kutoka Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho (IEC Lesotho) uliomtembelea Shambani kwake Zinje jijini Dodoma. Ugeni huo uliongozwa na Mjumbe wa Tume hiyo, Dkt. Karabo Mokobocho Monlakoana (katikati) na Mwenyeji wa msafara huo Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Asina Omar (wapili kulia). Wengine ni Watumishi wa Tume ya IEC Lesotho, Afisa Rasilimali watu,  Thato Moeti (wapili kushoto)  na Meneja Msaidizi wa Fedha Azael Limpho Monese. (Picha na Mroki Mroki).

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda (kulia) akizungumza na Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho (IEC Lesotho), Dkt. Karabo Mokobocho Monlakoana (katikati) na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Asina Omar wakati walipomtembelea Shambani kwake Zinje jijini Dodoma jana. Viongozi wa IEC Lesotho wapo nchini kwa ziara maalum ya kimafunzo ambapo pia walitembelea Ofisi za NEC.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda (wa tatu kushoto) akitoa maelezo ya namna ya ufugaji samaki wakati alipotembelewa shambani kwake na ujumbe wa Tume ya Huru ya Uchaguzi ya Lesotho, ulioongozwa na  Mjumbe wa Tume hiyo, Dkt. Karabo Mokobocho Monlakoana (wapili kushoto) Kushoto kwa Mzee Pinda ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Asina Omar aliyeambatana na ugeni huo.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda (kushoto) akitoa maelezo ya namna ya ulimaji wa kilimo cha zabibu wakati alipotembelewa shambani kwake na ujumbe wa Tume ya Huru ya Uchaguzi ya Lesotho, ulioongozwa na  Mjumbe wa Tume hiyo, Dkt. Karabo Mokobocho Monlakoana (kulia)  na katikati ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Asina Omar aliyeambatana na ugeni huo. (Picha na Mroki Mroki).

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com