![]()
![]()
Na. John Mapepele- WUSM
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohammed Mchengerwa amesema Wizara yake itahakikisha inafanya kazi kuanzia ngazi ya mitaa na vijiji ili kuleta mapinduzi makubwa katika sekta hizo katika kipindi kifupi.
Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo usiku wa ( Januari 14, 2022) kuamkia leo akiwa Mgeni Rasmi kwenye fainali za mashindano ya wa sanaa ya Bongo Star Search (BSS) 2022 jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wake, Dkt. Hassan Abbasi, na Naibu Katibu Mkuu, Said Yakubu
“Tunataka tuizungumze sanaa katika kila mtaa, tutaizungumza Sanaa katika kila kata, tutaizungumza Sanaa katika kila wilaya, na tutaizungumza Sanaa katika kila mkoa, tunataka Sanaa ndiyo iwe msingi wa kuendeleza katika kulinda na kuendeleza utamaduni wa taifa letu” amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Amesema kwa Wizara yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanakwenda kufanya mageuzi katika sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Aidha, amesisitiza kuwa yeye ni mtu wa kasi katika utendaji na matokeo zaidi hivyo atahakikisha kuwa matokeo makubwa yanapatikana katika Wizara yake.
Mhe. Mchengerwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake. Dkt. Hassan Abbasi kuona uwezekano wa kuwaendeleza washiriki wote wa shindano hilo katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo kilicho chini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza ni Bryson Yohana kutoka Dar es Salaam ambapo mshindi wa pili ni Andrew Charles kutoka Mwanza na mshindi wa tatu ni Suleiya Abdi mwanadada kutoka mkoa wa Dodoma.
Saturday, January 15, 2022
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe jana Tarehe 17 Juni 2019 aki...
-
HOTUBA YA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KATIKA JIMBO LA ISIMANI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI MWAKA 2015 UTANGULIZI UTA...
-
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe anautangazia Umma kuwa, Wizara imeandaa Mkutano wa Wafanyabi...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment