METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, January 15, 2022

JUKWAA LA BODI YA MAJI BONDE KATI LATAHADHARISHA TISHIO LA UHABA WA MAJI KUTOKANA NA UKAME

 


Wadau wa maji bodi ya maji bonde la kati wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa  jukwaa la pili lililofanyika  January 14 mkoani singida.

 


Mkurugenzi wa Rasilimali za maji Dkt. George Lugomela akitoa hutuba wakati  akimwakilisha katibu mkuu wizara ya maji katika kikao cha jukwaa la maji   bodi ya maji bonde la kati mkoani singida.


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa singida Alhaji Juma Kilimba akiwa katika kikao cha jukwaa la wadau wa maji bodi maji bonde la kati ilifanyika katika ukumbi wa  Bodi ya maji  bonde la maji zilizopo  mkoani singida.


Baadhi ya washiriki wa jukwaa la pili la wadau maji wa bodi ya maji bonde la kati  wakifuatilia mada mbalimbali zikitolewa wakati kikao kikiendeelea .


Na Hamis Hussein – Singida

WADAU wa jukwaa la  maji bodi ya maji bonde la kati wameitahadharisha jamii kutunza na kumia vizuri maji na vyanzo vyake ili viwasaidie hapo baadae kwa kuna kunauwezekano wa   kutokea kwa uhaba wa maji kutokana na uchache wa mvua  unaoendelea katika maeneo mbalimbali ambao ndio chanzo kikuu cha asili ya maji.

Wadau  hao wa maji wa bodi ya maji bonde la kati wakiwa katika Kupitia jukwaa la pili lililolenga kuandaa na kuidhinisha mipangokazi ya vikundi kazi ,  pamoja na mambo mengine wameisisitiza jamkii kutumia vizuri maji pamoja na kutunza vyanzo vya maji katika maeneo kwani uchache wa mvua uliojionyesha msimu huu unatishia kuwepo kwa kiwango cha maji ya kutosha ambapo mwenyekiti wa bodi za maji za mabonde  nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa bodi maji bonde la pangani Segule Segule amesema licha ya uchache wa maji uliopo hivi sasa jamii pia inapaswa kutumia vizuri maji

“ Hali ya maji kwa ujumla wake iko vizuri lakini kuna pahala pamekosa kidogo pengine pamepungua , sisi kama watu wa maji tunachokifanya tuanendelea kuhimizana  watumie kidogo kidogo  watambue kuwa kipindi cha ukame kimejitokeza sasa ” Alisema Segule Mwenyekiti wa Bodi za maji za mabonde  nchini

Aliongeza kuwa kama serikali kupungua kwa maji inatoa ishara ya kutengeneza miundombinu ya kutunza maji  kwa ujenzi wa mabwawa na miundombinu ya kuifadhia maji  kutokana maji mengi ya asili yatokanayo na mvua yanaenda kwenye maziwa  na mengine yanapotea .

Afisa maendeleo ya jamii mwandamizi wa bonde la kati Bi Nelea Bundala amesema hali ya maji kwa bonde hilo sio nzuri na huwenda ikasababisha migogoro ya maji kutokana nauhalibifu wa miondombinu ya maji kutokana asili ya jamii hiyo ambayo asilimia kuwa ni ya wafungaji  .

“Mwishoni mwa 2021 mpaka hapa tulipofikia  hali za rasilimali ya maji nchini sio nzuri  hususani bonde letu la kati tuna mikoa nane , mikoa hiyo ipo katikati ya nchi na inaongoza kwa idadi ya mifugo nchini asilimia 58 ya mifugo nchini inayopatikana na ukiangalia athali za kwenye vyanzo vya maji , ukame unazidi mabadiliko ya tabia nchi hali imeathiri vyanzo vya maji , mifugo imeanza kufa  na hali hii kama itaendelea hivi itaweza kuleta migogoro ya matumizi ya maji ” alisema Nelea Bundala Afisa maendeleo ya jamii mwandamizi  bodi ya maji bonde la kati .


Bi. Nelea Bundala Afisa maendeleo ya jamii mwandamizi bodi ya maji bonde la kati akielezea hali halisi ya upatikanaji wa maji kwa kipindi hiki cha ukame.


Mwenyekiti wa Bodi za maji za mabonde ambaye pia ni Mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la pangani Segule Segule Akitoa tahadhari ya kutumia maji vizuri pamoja na kutunza vyanzo vya maji kutokana na tishio la ukame msimu huu aliposhiriki katika jukwaa la pili la wadau wa maji bodi ya maji bonde la kati mkoani singida.


Lazaro Msagu  Mwenyekiti wa jukwaa  la wadau wa maji bodi ya maji bonde la kati Akitoa Ushauri wake kwa wanajukwaa kufanya tathmini ya namna ya kutafuta suluhu kulikomboa bonde hilo.

 

Hata hivyo Bi Nelea hakuishia hapo akataoa wito na pendekezo kwa wadau wote wa maji kupitia idara mbalimbali kutoa elimu kwa jamii namna ya kutunza vyanzo  vya maji ili viweze kusaidia katika kipindi hichi ambacho kuna tishio la ukame .

Kupotea au kupungua kwa maji katika maeneo mbali mbali kunachagizwa na  shughuli za kibinadamu kama vile kulima ndani ya vyanzo vya maji , uchenjuaji wa madini , utifuaji wa ardhi  nakadhalika Kaimu mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la kati danford Samson alitaja shughuli za hizo za binadamu zinavyoharibu vyanzo vya maji  na  kupelekea ukame.

“Upungufu wa sahivi unasababishwa na shughuli za kibinadamu kulimo ndani ya mita 60 , kufanyatua tofali kwenye  mito , uchenjuaji wa madini  hasa dhahabu mwenye vyanzo vya maji kama vile mito au ziwa” . Alisema Danford .


Kaimu MKurugenzi wa bodi ya maji bonde la kati Danford Samson Akifafanua baadhi ya mambo kwa waandishi wa Habari.


Wanajukwaa wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zikiwasilishwa kwenye jukwaa la pili la pili la wadau wa maji wa bodi ya maji bonde la kati

Mkurugenzi wa Rasilimali Za Maji Dkt. George Lugomela akimwakilisha katibu mkuu wa wizara ya maji  alisema jukwaaa la wadau wa bodi ya maji linapaswa kuunda majukwaa mengine madogo katika maeneo yao ya  ngazi ya chini  ili kurahisisha utatuzi wa changamoto za bonde la kati sanjari na kuwavutia wadau.

“Tunatakiwa tuendelee kuzindua majukwa ya bonde madogo ya maji au vidaka maji (catchment) hatuatikiwa kuishia kwenye mabonde ya kanda au la taifa  tuwende kwenye mabonde madogo  mfano hapa kwenu mna mabonde  madogo nane ziwa easi , natron  maana yake changamoto za easi na natron zitakuwa tofauti na mtaweza kujadiliana”. Alisema Dkt. Lugomela

Mwenyekiti wa jukwaa la wadau wa maji  bodi maji bonde la kati lazaro msagu amesema wao kama wadau wanapaswa kufanya tathmini ya namna ya kutatua changamoto za maji katika bonde hilo la kati  

Kwa mujibu wa jukwaa la wadau wa maji bodi ya maji bonde la kati  zaidi ya watu 200 wa bonde la kati wana maji lakini  hawana vibali  vya kutumia rasilimali hiyo jambo ambalo jukwaa limepaswa kuitatua changamoto hiyo .


Jukwaa la wadau wa maji bodi ya  maji bonde la kati  liliundwa  mwaka 2019 mara baada ya  kuanzishwa kwa  jukwa la wadu wa maji ya bonde la taifa 2017 ambapo katika kikao cha janury 14 mwaka huu kilijikita kuangazia majukwa mengine yaliopita sanjari na kupendekeza wajumbe wa bodi ya maji bonde la kati ambao wataenda kuchaguliwa na waziri wa maji.

 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com