METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, December 6, 2021

Shirika la FAO lakamia Usafi wa Mazao yaendayo Nje,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Dkt Njau atoa Muelekeo wa Mamlaka



Pichani: Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Dkt Efrem Njau akihutubia wadau wa kikao cha utekelezaji wa hatua za usafi wa mimea kwa upatikanaji wa Masoko(Picha zote na Innocent Natai)


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Dkt Efrem Njau akiteta jambo na Ndg.Mushobozi Baitani ambaye ni Afisa wa Afya ya Mimea FAO


Wadau wa kikao cha utekelezaji wa hatua za usafi wa mimea kwa upatikanaji wa Masoko ambao ni Mtaalamu wa Afya ya Mimea kutoka FAO, Maafisa kutoka mamlaka ya Afya ya Mimea na viuatilifu TPHPA,wakulima wa zao la Parachchi na wafanya biashara wa zao hilo,wakifuatilia hotuba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Dkt Efrem Njau 
 

Wadau wa kikao cha utekelezaji wa hatua za usafi wa mimea kwa upatikanaji wa Masoko ambao ni 
Mtaalamu wa Afya ya Mimea kutoka FAO, Maafisa kutoka mamlaka ya Afya ya Mimea na viuatilifu TPHPA,wakulima wa zao la Parachchi na wafanya biashara wa zao hilo,
wakifuatilia hotuba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Dkt Efrem Njau  

Na Innocent Natai  Arusha

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania,Dkt Efrem Njau amesema kuwa Mamlaka hiyo itaendela kutimiza wajibu wa Tanzania kwa mikataba ya kimataifa ya afya ya mimea kwa kuhakikisha inatoa mafunzo na kukagua mazao yanayosafirishwa nje ya nchi na yanayoingizwa nchini ili kudhibiti usafirishaji wa mazao yenye Visumbufu 

Dkt Njau ameyasema hayo hivi leo Tarehe 6 December 2021 hapa Mkoani Arusha wakati akifungua kikao cha utekelezaji wa hatua za usafi wa mimea kwa upatikanaji wa Masoko kilichoandaliwa na Shirika la FAO na kuwakutanisha Mtaalamu wa Afya ya Mimea kutoka FAO, Maafisa kutoka mamlaka ya Afya ya Mimea na viuatilifu TPHPA,wakulima wa zao la Parachchi na wafanya biashara wa zao hilo

Amesema kuwa Mwaka 2020, muongozo mpya wa udhibiti wa masuala ya afya ya mimea ulipitishwa kupitia sheria mpya ya Afya ya mimea ya mwaka 2020. Sheria hii iliunda Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu. Moja ya majukumu ya mamlaka hiyo ni kutimiza wajibu wa Tanzania kwa mikataba ya kimataifa ya afya ya mimea. Moja wa wajibu huo ni kuchukua hatua dhidi ya wadudu na magonjwa ya mimea yenye kusababisha nchi yetu kufungiwa masoko.

Ameongeza kuwa nchi ya Tanzania Hivi karibuni imekua ikifanya kazi na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, yaani FAO katika kufungua masoko ya parachichi ya India, Afrika Kusini, China na Marekani. Lengo letu ni kufungua haya masoko kwa masharti rafiki kwa biashara.

Tumefanikiwa kufungua masoko ya Afrika Kusini na India na kwa sasa tunaandaa mchakato wa kupunguza masharti ya kusafirisha parachichi kwenda India. Kila hatua tunayopiga ni ya muhimu. Wiki hii kupitia hii warsha, tutatoa muongozo utakaofanikisha kfunguliwa kwa soko la parachichi la China” Dkt Njau amebainisha

Ameongeza ameshukuru maafisa wa mamlaka ya afya ya mimea na viuatilifu (TPHPA) kwa juhudi zao kufanikisha hili. Pia shirika la FAO kwa mchango wao wa kitaalamu na uwezeshaji kwenye mchakato mzima na Umoja wa Ulaya kwa kuridhia kutoa takribani Shillingi Bilion 28 kwa ajili ya mradi wa kuimarisha huduma za afya ya mimea Tanzania. 

Aidha ameongeza kuwa Kupitia mradi huo watarekebisha maabara za Mamlaka na kuimarisha mifumo ya uchunguzi wa wadudu na magonjwa mashambani. 

Dkt Njau amesema ni matumaini yake kuwa washiriki wa Mkutano huo watazingatia yatakayotolewa na wataalamu na kuyafanyia kazi. 


Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com