Na Hamis Hussein - Singida
Wilaya ya Iramba mkoani Singida inatarajia kukabidhi jumla ya vyumba vya madarasa 61 ambavyo ni miradi ya elimu yenye thamani ya Sh. Bilioni 1.89 iliyojengwa kwa kutumia fedha za UVIKO 19 ifikapo tarehe Desemba 5, 2021.
Kauli
hiyo imetolewa Novemba 30, 2021 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
wilaya hiyo Michael Matomora alipokuwa
akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa
huo Dkt. Binilith Mahenge ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa
katika shule ya Sekondari Kyengege Kata ya Kyengege.
Aidha
amebainisha kwamba miradi yote imefikia hatua ya kupauliwa na tayari
wasafirishaji wapo Dar es Salaam kuchukua mabati ambapo tunatarajia ndani ya
siku mbili au tatu yatakuwa yamefika katika maeneo ya kazi, hivyo ni imani yetu
kwamba mpaka tarehe tano tutakuwa tumemaliza kupaua kwa sababu tumesha nunua
kila kitu, Alisema Matomora.
Mkurungezi
huyo akabainisha kwamba katika miradi hiyo 47 ni ya ujenzi wa madarasa katika
Shule za Sekondari 19 ambazo zitagharimu kiasi cha sh.Milioni 940
Aidha
Mkurugenzi huyo akaeleza kwamba miradi 14
ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 14 katika shule shikizi saba (7)
ambazo ni Ulongo, Magugu, Kagera, Itunda, Masunkune, Kisingu na Ibambasi
ambazo zitagharimu kiasi cha Tsh. Milioni 280.
Amesema
kwa ujumla Shule ambazo zinatekeleza miradi ya UVIKO 19 katika wilaya ya Iramba
ni Lulumba, New Kiomboi, Kinambeu, Shelui, Kyengege, Kizaga, Kidaru, Mbelekese
na Mtekente. Nyingine ni Mtoa, Tulya, Ntwike, Urughu, Ushora, Kinampanda, Mukulu,
Mgongo, Kaselya na Kisiriri. alifafanua Matomora.
Akijibu
baadhi ya changamoto zilizojitokeza kwenye utekelezaji wa miradi hiyo ikiwemo
baadhi ya wakuu wa Shule kutotizimiza majukumu yao vizuri Mkuu wa Mkoa Dkt.
Mahenge amesema Serikali haitamvumilia mtumishi yeyote wa Serikali atakaye
sababisha uzembe katika utekelezaji wa miradi hiyo.
“Yeyote atakayefanya
uzembe wa makusudi tutamchukulia hatua za kinidhamu ili iwe fundisho kwakwe na
wengine wenye tabia kama hizo, lengo likiwa sio kumkomoa bali ni kwa ajili ya
manufaa ya jamii husika”.
Alisema Dkt. Mahenge.
Hata
hivo RC Mahenge amewapongeza
viongozi wa wilaya ya Iramba kwa
jitihada zao katika kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo ambapo mpaka sasa
madarasa yote yamefikia hatua ya
kupaliwa.
Aidha
RC. Mahenge akawataka viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba pamoja na
viongozi wa CCM kuendelea kusimamia kazi hizo na kuhakikisha kwamba inakamilika
kabla au ndani ya Desemba 5, 2021.
Awali
Suleiman Mwenda akimkaribisha Mkuu wa mkoa alisema wilaya inatekeleza miradi 47
ya ujenzi wa madarasa katika shule 19
ambapo jumla ya madarasa 18 yamefikia hatua kupauliwa katika shule saba (7)
0 comments:
Post a Comment