Na Hamis Hussein- Singida
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge Novemba 30, 2021 amezindua Rasmi na kukabidhi basi aina ya Coasta kwa ajili ya
kusafirishia wafanyakazi wa Hospitali ya Mandewa iliyopo mkoani hapo kama
kitendea kazi kitakachowasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.
Akiongea
na wafanyakazi akiwa Hospitalini hapo baada ya kuwakabidhi basi Mkuu wa Mkoa
amewapongeza watumishi kwa namna ambavyo wamekuwa wakifanya kazi katika
mazingira magumu na wengi wao wakitumia
bodaboda kufika kazini lakini pia hawakukata tamaa.
RC
Mahenge amemtaka Afisa usafirishaji wa Hospitali ya mkoa wa Singida kuhakikisha
kwamba basi hilo linatunzwa na kuzingatia muda wa kufanyia huduma (service) kila inapofika muda
wake ili kulifanya lidumu kwa muda mrefu na kuendelea kuwasaidia watumishi.
Amewataka
madaktari katika hospitahi hiyo ambayo ni Tawi la Hospitali ya Mkoa wa
Singida kuboresha huduma zao na
kuzifanya ziwe za kibingwa ili kuifanya
Singida kuwa kimbilio la mikoa ya jirani
(center of excellence )
Aidha
ameitaka bodi ya Hospitali hiyo kuanza kufikiria namna ya kujenga nyumba za
watumishi kupitia vyanzo vyao vya ndani au kupitia mashirika mbalimbali kwa kuwa kukaa karibu na hospitali kunaongeza
ufanisi katika kazi.
Akimalizia
hotuba yake mkuu wa mkoa amewataka madaktari hao pamoja na bodi kuyafanya
majengo ya zamani kuwa hospitali ya Wilaya halafu majengo ya Hospitali ya
Mandewa yatumike kama hospitali ya mkoa.
Awali
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa Dkt. Deogratius Banuba akisoma hotuba yake
amesema gari hilo lina thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 236 ambazo zilitokana na
makusanyo ya ndani.
0 comments:
Post a Comment