METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, November 11, 2021

ASA KUWEZESHA MAAFISA UGANI 630 KUTOKA KATIKA MIKOA YA DODOMANA SINGIDA

 Mkurugenzi wa Mafunzo huduma za ugani na utafiti kutoka wizara ya kilimo Dkt , Wilhelm Mafuru kushoto akikabidhiwa mfuko wa Mbegu za Alizeti na mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA, Dkt, Sophia Kashenge kulia wakala wametoa Tani mbili za Alizeti kwa maafisa ugani wa mikoa ya Dodoma na Singida. 

Na Lucas Raphael,Morogoro

Maafisa ugani 630 kutoka  mikoa ya singida na Dodoma wanatarajia kuandaa mashamba darasa ya Alizeti ili wakulima waweze kujifunza kupitia mashamba hayo.

Akizingumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Mafunzo huduma za ugani na utafiti Dkt , Wilhelm Mafuru alipotembelea makao makuu ya Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Jana alisema maafisa hao watatakiwa kila moja awe na Shamba darasa ili wananchi wa eneo husika waweze kujifunza.

Alisema Ziara yake fupi kwa Wakala wa Mbegu ni kwa ajili ya kushuhudia na kujifunza uandaaji wa mbegu hizo na hatimaye kuchukua  Mbegu za Alizeti ambazo zitasambazwa kwa maafisa ugani wa mikoa hiyo ya dodoma na Singida.

Alisema lengo la wizara kufanya hivyo ni kuhakikisha wakulima wanalima kilimo sahihi kwa kufuata taratibu na kanuni za zao la Alizeti ili wapate mazao mengi yatakayo punguza tatizo la mafuta Nchini.

Alisema serikali inatumia pesa nyingi kuagiza mafuta hivyo wizara ya kilimo imeliona Hilo na mikakati mbalimbali inaendelea ya kuhamasisha wananchi kulima mazao ya mafuta hasa Alizeti ambayo maeneo mengi hapa Nchini inastawi nakutoa mazao mengi.

Akizungumzia ufanisi wa Wakala Dkt. Wilhem Mafuru alisema Wakala umeongeza ufanisi wa kazi zake ukilinganisha na.miaka kadhaa iliyopita hasa katika Uzalishaji wa Mbegu, Uchakataji, uandaaji pamoja na vifungashio. Hali inayoonekana kazi kubwa  inafanyika kulingana na maelekezo ya wizara na uhitaji wa jamii.

Alisema Wakala chini ya uongozi wa mkurugenzi wake Dr. Sophia Kashenge kazi inaonekana vile vile  uwajibikaji umeongezeka tofauti na hapo awali. Kwa sasa Wakala anaanza kulimudu soko la Mbegu  pamoja kukazana kutatua changamoto ya upatikanaji wa Mbegu. Tunawapongeza sana

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo Tanzania ( ASA) Dkt. Sophia Kashenge alisema Suala la kushughulikia upatikanaji wa mbegu za alizeti ni moja ya mambo yanayopewa kipaumbele kitaifa kupitia wizara ya Kilimo. Jukumu letu sisi kama ASA ni Utekelezaji  wa maelekezo tuyopewa na kuhakikisha tunapunguza changamoto ya upatikanaji wa mbegu za alizeti”.

Hata hivyo Dkt, Kashenge aliipongeza wizara ya kilimo kupitia waziri wa kilimo na Naibu Waziri wa kilimo pamoja na makatibu wakuu kwa kuhakikisha zoezi Hilo la kusambaza Mbegu Nchini linafanikiwa.

Alisema Kwa sasa changamoto kubwa wanayo kutananayo  ni  usafirishaji wa Mbegu kwa wahitaji ambapo changamoto hiyo wanaendelea kufanyia kazi kwa kuongeza mabehewa ya treni iliu safilishaji ufanyike kwa haraka.

Aidha  Dkt, Kashenge  amewashukuru watumishi wa ASA kwa kujituma kwa dhati katika kufanikisha  zoezi hili la uandaaji na Uchakataji wa Mbegu linakamilika.

Alisema wanafanya kazi mpaka asubuhi lengo ni kufanya kila wanaloweza Ili Mbegu zifike ndani ya msimu kwa wakulima nakuongeza kuwa Mbegu hizo zinauzwa kwa Bei nafuu.

Akitoa Wito kwa wakulima Dkt,Sophia Kashenge amewataka watumie mbinu bora za kilimo Ili kupata tija ya Uzalishaji inayotarajiwa katika Mbegu hizo.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com