Waziri wa kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akiwa ameambatana na Waziri wa Mazingira, Kilimo na Uvuvi wa Burundi Mhe. Dkt Rurema Deo-Guide wakikagua baadhi ya mazao ambayo yamefanyiwa utafiti na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Nchini Burundi ya Isabu, Tarehe 20 Octoba 2012.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Burundi
Tanzania
ina uhusiano mzuri na majirani wake na katika miaka ya hivi karibuni imekuwa
mshiriki kwa ukamilifu katika juhudi za kuhimiza usuluhilishi wa migogoro kwa
njia ya amani.
Tanzania
ni mwanachama wa vikundi vya kimataifa na kikanda pia inashiriki kwa dhati
katika ushirikiano wa baina ya nchi na ushirikiano wa kimataifa.
Tanzania
pia ilisaidia mazungumzo ya amani kumaliza mgogoro nchini Burundi ambapo mazungumzio hayo yalifanyika Jijini Arusha.
Serikali
ya Tanzania imeendelea na juhudi zake za kuimarisha ushirikiano na nchi jirani ikiwemo
Burundi ambapo pamoja na mambo mengine imekusudia kuimarisha ushirikiano katika
sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo.
Kufuatia ushirikiano huo Waziri wa kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda amefanya ziara ya kikazi nchini Burundi ambapo aliwasili Tarehe 18 Octoba 2021 na kuanza ziara ya siku mbili tarehe 19-20 Octoba 2021.
Pamoja
na mambo mengine katika ziara hiyo Waziri Mkenda amekutana na kufanya
mazungumzo na mwenyeji wake amekutana
na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mazingira, Kilimo na Uvuvi wa Burundi Mhe.
Dkt Rurema Deo-Guide
Akizungumza
mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Ngozi na Kayanza
alipotembelea kujionea mashamba ya Kilimo cha mahindi (Block Farming) pamoja na
kutembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Nchini Burundi ya Isabu, Waziri
Mkenda amesema kuwa lengo la ziara yake katika maeneo hayo ilikuwa ni kujionea
hali ya ubora wa mazao ya wakulima yanayotumia mbolea ya FOMI.
“Tumekutana
na wanasayansi wa hapa Burundi ili kuzungumza nao waweze kutueleza kuhusu
utafiti walioufanya wa mbolea ya FOMI ili kujiridhisha kabla ya kuingia
makubaliano ya kuanza matumizi ya mbolea hiyo kule nchini kwetu” Amekaririwa
Waziri Mkenda
Waziri
Mkenda amemuhakikishia mwenyeji wake ambaye ni Waziri wa Mazingira, Kilimo na
Uvuvi wa Burundi Mhe. Dkt Rurema Deo-Guide
Amesema
kuwa viongozi wakuu wa nchi zote mbili Tanzania na Burundi wamekuwa wakijenga
uhusiano mzuri wa Kidiplomasia na kisiasa kwani wananchi wameendelea kufanya
biashara za mazao bila vikwazo hususani mazao ya mahindi, mchele na Parachichi.
“Tuna
kazi kubwa sisi kama serikali kuimarisha mahusiano makubwa ya kibiashara na
uchumi kama ambavyo viongozi wetu wanafanya, nasi tumekubaliana kushirikiana
katika sekta ya utafiti wa mazao” Amesisitiza Waziri Mkenda
MWISHO
0 comments:
Post a Comment