Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndugu Christina Mndeme amewataka wananchi wa Ruangwa mkoani Lindi kushiriki kikamilifu pindi Sensa itakapowafikia mwaka 2022.
Akizungumza na wakazi wa shina namba 8, Namichiga, Ruangwa mkoani Lindi,
Mndeme Alisema “Sensa ikifika tujitokeze tuhesabiwe inakuwa rahisi kwenye mipango ya maendeleo”.
Pamoja na mambo mengine katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), amewasihi wananchi hao kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Mkuungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwani amedhamiria kuleta maendeleo makubwa nchini.
Naibu Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoani Lindi yenye lengo la kukagua na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
0 comments:
Post a Comment