Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Moyo akijibu baadhi ya kero za wananchi wa tarafa ya Kiponzero alipokuwa kwenye ziara yake ya kusikiliza kero vijiji na mitaa yote ya wilaya hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Moyo akijibu baadhi ya kero za wananchi wa tarafa ya Kiponzero alipokuwa kwenye ziara yake ya kusikiliza kero vijiji na mitaa yote ya wilaya hiyo
Baadhi ya wananchi wa tarafa ya Kiponzero wakimsikiliza na kutoa kero zao kwa mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo
Baadhi ya wananchi wa tarafa ya Kiponzero wakimsikiliza na kutoa kero zao kwa mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wanaume Wilayani Iringa yaiomba Serikali kuwanusuru na vitendo vya ukatili wanavyotendewa na wake zao ikiwemo kupigwa na kudharirishwa hali inayowaathiri kisaikolojia na kiuchumi vitendo wanavyovitaja kuchangia baadhi yao kukimbia na kutelekeza familia kwa kuhofia usalama wao na aibu katika jamii.
Wakizungumza katika Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo yenye lengo la kubaini kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi baadhi ya wanaume wa tarafa ya Kiponzero wamesema iko haja ya kuwapo kwa dawati maaalum la utetezi wa haki za wanaume na usaidizi wa kisaikolojia ili kuwaepusha na msongo wa mawazo kutokana na ukatili huo.
Miongoni mwa wanaume hao Walimueleza Mkuu wa Wilaya wake zao wamekuwa na tabia ya kuwafanyia ukatili wa namna hiyo mara kwa mara lakini jambo la kushangaza baadhi yao wanapotoa taarifa kwa viongozi wa Serikali za vijiji na kata ili kupata usaidizi hawaoni hatua za moja kwa moja kuchukuliwa,
Alisema kuwa hatua inayosababisha baadhi yao kutafuta namna za kukabiliana na ukatili huo hali inayopelekea kutenda uhalifu mkubwa zaidi wakati wa kulipa kisasi na kusababisha kuongezeka kwa ukatili katika jamii.
Wanaume hao walisema kuwa baadhi yao wamekuwa wanashindwa kutoa taarifa za vitendo hiyo vya unyanyasaji wa kijinsia kutokana na mila na desturi za watanzania kuwa mwanaume kupigwa na mwanamke ni aibu kubwa katika maisha.
“Kwa kweli sisi wanaume tunapigwa sana, yaani tunafanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na tunashindwa kutoa Taarifa kutokana na mila zetu sisi wahehe” walisema wanaume hao.
Aidha wanaume hao wameiomba serikali kuingilia kati kuhusu vitendo hivyo kwani vimekithiri katika tarafa ya Kiponzero na kunasababisha kuwanyima haki za msingi baadhi ya wanaume ambao wamekuwa wanafanyiwa vitendo hivyo.
Akijibia changamoto ya Wanaume kupigwa kwa Niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Iringa (OCD), Afande Agustino Malema ambaye ni mkuu wa Kituo cha Polisi Ifunda alisema kuwa jeshi la polisi limeanzisha kitengo cha dawati la jinsia ambalo linahusika na matukio kama hayo.
Alisema kuwa hakuna mtanzania au mwananchi yeyote yule anayetakiwa kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsi kwa kuwa mara nyingi kitendo hicho kimekuwa kikiwaathiri kisaikolojia na kupunguza ufanisi wa akili zao.
Afande Malema alisema kuwa wananchi wote wanaofanyiwa vitendo hivyo wanatakiwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi bila aibu ili kumaliza tatizo hilo ambao limekuwa linaibuka kwa kasi kwa kipindi cha miaka ya hizi karibuni.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Moyo alisema kuwa moja ya agenda yake katika ziara yake ni kutoa elimu ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa wananchi wote wa wilaya hiyo ili kuondoka katika nafasi waliyopo.
Moyo alisema kuwa mkoa wa Iringa na wilaya ya Iringa vinaongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo ni lazima watafute njia ya kukomesha vitendo hivyo ambavyo vinakuwa vikiharibu sifa kubwa ambayo wilaya hiyo inayo.
Mkuu wa wilaya huyo aliwaagiza wenyeviti wa vijiji na watendaji kuhakikisha wanavifichua vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia ili kuwaondoa waathirika katika msongo wa mawazo ambao wanakumbana nao mara baada ya kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia
Alisema kuwa kitendo cha kumpiga mtu ni kosa la Jinai hata kama amefanya kosa huku akiwataka wananchi wa kijiji hicho kwenda kuripoti matukio hayo ya ukatili wa kijinsia katika vyombo vinavyohusika.
0 comments:
Post a Comment