Pichani: Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda (Picha na Maktaba yetu)
Na Jackline Kuwanda, Dodoma.
Waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema nchi inakabiliwa na uhaba wa maafisa ugani ,ambapo hadi kufikia mwaka 2019/2020 kulikuwa na jumla ya maafisa ugani 6704 sawa na 33% ya mahitaji yote
Profesa Mkenda ameyasema hayo leo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma wakati akizindua Mafunzo Rejea ya Kilimo Bora cha Alizeti kwa maafisa ugani, ambapo amesema mahitaji ya maafisa hao ni 20,538.
‘’hivyo utendaji wa kazi katika mazingira haya unahitaji kuongeza ubunifu na maarifa kuweza kuwafikia wakulima wengi zaidi’’ amesema
Wakati huo huo, Profesa Mkenda amesema katika kukabiliana na uhaba wa changamoto ya maafisa hao, wizara imeanzisha mfumo wa kidigitali ambao unawezesha wakulima kutumia simu zao kuwasiliana na maafisa hao kuomba huduma za ushauri na kupata taarifa masoko.
‘’Nawaombeni tumieni mfumo huu utasaidia sana kuwafikia wakulima wengi katika hali hii ya uhaba wa maafisa ugani’’ amesema
Kwa upande wake , Mkurugenzi wa Mafunzo ya Huduma za Ugani na Utafiti Wizara ya Kilimo Dkt Wilhelm Mafuru, amesema mafunzo hayo ya awamu ya kwanza yatashirikisha maafisa ugani 270 kutoka katika halmashauri 18 za mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara .
‘’na itaendelea katika mikoa mingine ikiwemo Mkoa wa Simiyu kwaajili ya lile zao la pamba ,kituo cha mpwapwa kinajumuisha washiriki 51 kutoka halmshauri za Mpwapwa,kongwa na Bahi, ambapo Mpwapwa kutakuwa na washiriki 24,Kongwa 12 Kongwa, Bahi 15 pamoja na sektreatieti kutoa mshiriki mmoja’’ amesema
0 comments:
Post a Comment