Waziri wa Kilimo, Mhe Prof.
Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo
Maafisa Ushirika yaliyofanyika katika ukumbi wa BOT mkoani Mtwara, tarehe
20 Septemba 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu Waziri wa Kilimo,
Hussein Bashe akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea
uwezo Maafisa Ushirika yaliyofanyika katika ukumbi wa BOT mkoani Mtwara, tarehe 20 Septemba 2021.
Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe Hassan Mtenga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo
Maafisa Ushirika yaliyofanyika katika ukumbi wa BOT mkoani Mtwara, tarehe 20 Septemba 2021.
Mrajis wa Vyama Vya Ushirika,
Dkt. Benson Ndiege akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya
kuwajengea uwezo Maafisa Ushirika yaliyofanyika katika ukumbi wa BOT mkoani
Mtwara, tarehe 20 Septemba 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Ushirika yaliyofanyika katika ukumbi wa BOT
mkoani Mtwara, tarehe 21 Septemba 2021.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara
Waziri wa Kilimo Prof Adolf Mkenda ametoa onyo
kali kwa wanunuzi wa korosho kwa njia isiyo halali maarufu kama 'Kangomba' hali
inaweza kusababisha wakulima kushindwa kuendelea kulima zao hilo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya maafisa ushirika yanayojumuisha mikoa mitano yanayofanyika mkoani mtwara amesema kuwa lazima wakemee ili kumsaidia mkulima.
Amesema kuwa serikali ina mikakati ya
kuwezesha wakulima ili waendelee kulima zao hilo ambapo wanatoa pembejeo na
kuwawezesha kwa namna mbalimbali ikiwemo kuimarisha ushirika na kuwawezesha
maafisha ushirika na ugani ili kuwezesha zao hilo kuendelea kufanya vizuri.
“Hivi mnajua kuwa kangomba imerudi tena
imerudi kwa kasi kwelikweli kwenye korosho tuwalinde wakulima kangomba
inawapiga kwelikweli tusaidiane kuhimiza wakulima wasiuze kangomba tunawaacha
wanaziuza hovyo hii inaua zao la korosho”
“Maafisa ushirika jiulizeni nini kinaleta
kangomba je ni tamaa ya fedha au nini? Kwanini tusije na mkakati ambao
utamsaidia mkulima asiuze kangomba tu aipinge na kuizuia kwa nguvu zote lakini
tunamsaidiaje mkulima ili akiwa na mahitaji yenye mashiko achukue pesa kwenye AMCOS
kama ilivyo kwa wafanyakazi huwezi kuendesha uchumi kwa mijeredi lakini hili
jambo tusipolishikilia tutaua zao la korosho tuanze mikakati ya kujenga SACCOS
ili kuwasaidia wakulima wa zao la korosho wasiuze kangomba” amesema Mkenda
Katika hatua nyingine Waziri huyo amekemea
chama cha ushirika kilichopo Nanjilinji Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi kilichouza
ufuta wa wakulima na kukaa na fedha za wakulima.
“Huo ni utapeli na hiyo ni jinai unawezaje
kuchukua fedha za mkulima kisha ukaa nazo bila kumkabidhi mkulima lazima hatua
zichukuliwe ningekuwa na uwezo ningesukuma ndani hawa kimsingi wanatuhatibia
ushirika”
“Huwezi kumkopa mkulima wewe nani unazunguka
na pesa ili iweje haya ni matokeo ya wakulima wachache kuwepo kwenye ushirika
ambao wamekuwa wakiamua hatma ya uuzwaji wa mazao ya wakulima wengi ambao
hawapo kwenye umoja huo”
“Ubadhirifu chama cha msingi Nanjilinji kilwa
tutawashugulikia wamenunua ufuta kwa wakulima wanazunguka na fesha za wakulima
tutawachukulia hatua, hizo fedha ni za wakulima wachache wameweka utaratibu
lazima mazao yapitie kwenye ushirika” amesema Mkenda
Nae Mrajis Mkuu wa Vyama vya Ushirika nchini
Dkt Benson Ndiege amesema kuwa mafunzo hayo yanajumuisha vyama zaidi ya 9000
nchini ambapo zaidi ya maofisa 400 watajengewa uwezo.
“Tunahitaji kujenga ushirika mpya nchini ili
tufanye mabadiliko kwenye ushirika ili tuwe na watu wenye uwezo wa kufanya
kaguzi wenyewe kabla hawajakaguliwa mfano mwaka 2019/20 ukaguzi ulifanyika
chini ya asilimia 60 lakini maofisa wenye uwezo wa kujikagua walikuwa 33 lakini
pia hawakujikagua ndio maana tunawajenga uwezo ili waweze kujikagua wenyewe na
kuwapa vitendea kazi”
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga amesema kuwa vyama vya ushirika vimekuwa sehemu ya utendaji kazi usio na maadili ambao una fifisha jitihada za wakulima huku ubadhilifu wa fedha ukitajwa kwa kiasi kikubwa kutokea katika vyama hivyo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment