METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, September 13, 2021

MATUMAINI MAKUBWA, TANZANIA KUIMULIKA NA KUANGAZA E.A NA AFRICA.




Na: Jesca Kishoa

Jana nimeshuhudia kasi kubwa na nzuri iliyofikia 82%  ya ujenzi wa mradi wa umeme Rusumo (MW 80) unaojumuisha nchi 3 Rwanda, Burundi na Tanzania. 

Kwa ufupi kufikia mwaka 2022 miradi miwili ya uzalishaji wa umeme Rusumo na Rufiji ikikamilika na kuanza kazi Tanzania tutaweka record kubwa Africa kwa uzalishaji mkubwa wa umeme zaidi ya  MW 3700,  ambapo katika hizi makadilio yanaonyesha  Tanzania kwa siku itatumia karibu *MW 1300 tu kwa utoshelevu nchi nzima bila mang'amun'gamu.  Umeme unaobaki utaweza kuuzwa nje na tukaingiza mapato serikalini. Na kama Kufikia 2025  miradi yote ya kufufua umeme ikikamilika tutakuwa na MW 5000. 

Ukiachana na TZ kuizidi Nigeria yenye MW.3000 ambapo Nigeria ni nchi inayoongoza kwa uchumi mkubwa Africa, Tanzania  Kwa upande wa East Africa tutaendelea kuwa   vinara wakuu tukifatiwa na Kenya MW. 2217, Uganda MW.964, Rwanda MW. 211 na Burundi MW.41. 

Tusidanganyane hakuna nchi Duniani imewahi kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi (viwanda) bila umeme wa uhakika, unaotosheleza, unaotabirika na wagharama nafuu.

Hii ni hatua kubwa na nimafanikio makubwa tunayoyatarajia ni vema wananchi kujua ukubwa huu jambo hili na kujivunia tu na kulinda miundombinu ya miradi hii kwa wivu mkubwa.

Kikubwa na muhimu kwa sasa ni kuhakikisha wananchi wa maeneo hayo wamelipwa fidia zao ili kuepusha mivutano na kuondoa ladha nzuri ya uzuri wa uwekezaji huu mkubwa.

 Pia ni vema sana serikali   kuendelea kuzingatia Energy mixing ili tuwe na vyanzo tofauti vya kuzalisha umeme. Kama mikakati iliyoandaliwa itazingatiwa kama ilivyo kwenye taarifa za wizara basi tunategemea mbeleni tutakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme kutoka gesi 60% , maji 75% , na vyanzo vingine 24% . Hii itasaidia kuwa na vyanzo tofauti na itashusha gharama .


Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com