METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, September 14, 2021

DC MOYO: WAZAZI WA WANAFUNZI WALIOPATA MIMBA KUSAKWA POPOTE WALIPO

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Luhota juu ya madhara ya mimba za utotoni kwa wanafunzi wanaosoma katika shule zote za kata hiyo
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Luhota juu ya madhara ya mimba za utotoni kwa wanafunzi wanaosoma katika shule zote za kata hiyo



Na Fredy Mgunda,Iringa.

 Mkuu wa wilaya ya Iringa ameagiza kukamatwa kwa wazazi wa wanafunzi wane waliopata ujauzito katika shule ya sekondari Luhota wakijumuishwa na wazazi wa watoto wa kiume waliowapa ujauzito ikiwa ni hatua ya kukomesha vitendo vya kuwaficha wanaotuhumiwa na vitendo hivyo.

Hatua hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa imekuja kufuatia taarifa iliyotolewa na baadhi ya wazazi katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika vijiji vya Tagamenda na Kilambo baada ya wazazi hao kudai kuwa wanafunzi wa kike wamekuwa wakiacha mimba kutokana na kupata ujauzito wakiwa shuleni.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara baadhi ya wazazi hao walisema kuwa wanafunzi wengi wa kikke katika kata ya Luhota wamekuwa hawazifikii ndoto zao kutokana na kukatisha masomo mara baada ya kupata ujauzito wakiwa mashuleni na hakuna hatua za kisheria ambazo zimekuwa zikichukuliwa kwa watuhumiwa.

Wazazi hao walisema kuwa wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule ya sekondari ya Luhota wamekuwa na asilimia ndogo ya kumaliza masomo yao kutokana na wanafunzi hao kukumbana na vishawishi vingi wanapoenda shule ni kusoma.

“Moja ya sababu zinazopelekea changamoto hiyo ni umbali Mrefu wa naotembea watoto kufuata shule pamoja na kutochukuliwa hatua kwa watu wanaohusika na mimba hizo hatua hiyo inayochechea kulichukulia jambo hilo la kawaida na kuzoeleka kwa wananchi wa vijiji vya kata ya Luhota” walisema wazazi

Aidha wazazi hao walimuomba mkuu wa wilaya ya Iringa kuhakikisha wanawachukulia hatua kali wanaume wote ambao wamekuwa wanawapatia ujauzito wanafunzi hao kwa kuwa kufanya hivyo ni kama kosa la jinai na watu hao wanatamkiwa kufungwa kwa mujibu wa sharia na katiba ya nchi inavyotaka.

Akielezea kuhusiana na matukio ya wanafunzi hao kupata ujauzito wakiwa shuleni, Mkuu wa Shule ya Sekondari Luhota iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Lesiyo Kisonga kuwa jumla ya wananfunzi wanne wamepata ujauzito katika kipindi cha mwezi wa kwanaza hadi mwezi wa tisa jambo lililowapelekea kufukuzwa shule kwa mujibu wa sheria za nchi.

Alisema kuwa changamoto ya wanafunzi wengi imekuwa inajitokeza mara kwa mara kutokana na wazazi kushindwa kutoa ushahidi katika mamlaka husika baada ya watoto wao kugundulika kuwa wamepata ujauzito wakiwa shuleni jambo ambapo limepelekea wanaume wengine kuwa jambo hilo ni la kawaida kwao.

“Moja ya changamoto zinakwamisha mapambano ya kuzuia mimba shuleni ni kukosekana kwa ushahidi na ushirikiano kutoka kwa wazazi na watoto wenyewe kukataa kumtaja mhusika wa ujauzito ambao amekuwa amepewa na wanaume huyo” alisema Kisonga

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo aliliajiza jeshi la polisi wilaya ya Iringa kuhakikisha wanawakamata wazazi wote wa wototo wanne waliwapatia ujauzito na watoto wenye ujauzito kwa lengo la kukomesha matukio hao.

Alisema kumekuwa na wazazi ambao wamekuwa wanafanya makubaliano kifamia huku wakiwa wanakatiza ndoto za wananfunzi hao wa kike hivyo lengo la kuwakamata wazazi hao wote ili kupunguza na kumaliza tatizo la kuwapatia ujauzito wanafunzi hao.

Moyo alisema kuwa lengo la kuwakamata wote hao ni kuhakikisha ushaidi haupotei wala keshi hizo haziishii ngazi za familia kama ambavyo inafanyika hivi sasa kwenye jamii nyingi za wananchi wa wilaya ya Iringa na kusema kuwa Iringa bila mimba za utoto inawezekana.

Aliwataka viongoziwa vijiji,mtaa,kata na tarafa kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi ili kukamilisha ushaidi wa keshi hizo na kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa lengo la kumaliza tatizo la mimba za utotoni.

Jumla ya Mimba nne zinatajwa kutokea katika kipindi cha mwezi January hadi September mwaka huu jambo linalorudisha nyuma ndoto za watoto wa kike.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com