METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, December 10, 2020

WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MENEJIMENTI YA OFISI YA WAZIRI MKUU JIJINI DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kipokelewa rasmi na watumishi wa ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma hii leo Disemba 10, 2020.

Sehemu ya Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Vitengo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia kwa makini maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) mara baada ya kuwasili ofisini hapo.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidi taarifa ya Utekelezaji Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kupokelewa rasmi katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akieleza jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Vitengo mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidi taarifa ya Utekelezaji Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi wakati wa kikao hicho.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com