Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Iringa
Serikali imekamilisha mazungumzo
na kampuni ya ubia ya Sudani ya Kusini kwa ajili ya kuuza unga pamoja na mtama
mweupe.
Hiyo ni fursa kubwa kwa
wafanyabiashara nchini kwani wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo ambayo itakuwa
sehemu ya muarobaini wa soko la nafaka kwa wakulima nchini.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof
Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 2 Agosti 2021 mjini Iringa mara baada ya
kutembelea na kukagua kinu cha usagishaji nafaka cha Bodi ya Nafaka na Mazao
Mchanganyiko (CPB).
Kuhusu kadhia ya uzalishaji
duni wa mazao mbalimbali hususani nafaka Waziri Mkenda amesema kuwa serikali
inaendela kutoa elimu kwa wakulima kuhusu kuongeza tija kwenye mazao kadhalika
kuongeza uzalishaji.
“Kuna uwezekano wa kuzalisha gunia
40 katika hekari moja hivyo ni lazima tuweke msisitizo kwenye kuongeza
uzalishaji na tija” Amekaririwa Waziri Mkenda
Amesema kuwa pamoja na
kuongeza tija na uzalishaji lakini ili kufikia hatua kubwa katika uzalishaji na
tija hivyo ni lazima kuimarisha sekta ya mbegu na kuwa na upatikanaji wa mbegu
bora nchini.
Kuhusu bei ya mahindi, Prof
Mkenda amesema kuwa bei ya mahindi iliporomoka hivi karibuni ambapo aliagiza
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao
Mchanganyiko (CPB) kuingia sokoni ili
kununua nafaka hususani mahindi jambo ambalo limeanza kuimarisha bei ya mahindi.
Katika ziara hiyo ya Waziri
wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda kwenye mikoa ya Nyanda za juu kusini imejikita
katika kugagua hali ya upatikanaji wa mbolea, ununuzi wa mahindi pamoja na
kukagua skimu za umwagiliaji.
MWISHO
Safi sana
ReplyDeleteSafi sana. Maisha ya mkulima lzima yainuke. Hongereni
ReplyDeleteSafi sana
ReplyDeleteHongera Sana waziri tunaomba pia mipunga itoke nje maana wakulima wa mipunga tunahangaika Bei iko chini Sana
ReplyDelete