Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na TAMISEMI, Sekretarieti za
Mikoa na Halmashauri za Serikali za Mitaa zinaendelea na usajili wa wakulima
kwenye mfumo wa M-Kilimo ili waweze kutambuliwa, kutoa huduma kwa njia ya
simu na pia Serikali kutoa huduma zingine kwa urahisi.
Mpaka sasa hivi zaidi ya nusu ya mikoa yote Tanzania Bara, Mikoa
14 imeweza kusajili na kufikia asilimia 50 au zaidi kwenye mfumo huo wa
M-Kilimo.
Akizungumzia hali ya usajili wa wakulima mpaka hivi sasa, Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Prof. Siza Tumbo amesema kuwa Mikoa 12 bado
ipo chini ya asilimia 50 kwenye usajili wa wakulima.
Prof. Tumbo ameeleza kuwa Mikoa minne (4) ambayo ni Njombe,
Arusha, Simiyu na Singida imeweza kufikia lengo la asilimia 100 na zaidi.
Wizara ya Kilimo inaipongeza sana mikoa hii kwa kufikia hatua hiyo.
Amesema kuwa Mikoa ya Shinyanga, Kagera na Dar-es-Salaam bado
wapo chini ya asilimia 30, hivyo kuwasihi kuongeza kasi ili kufikia malengo ya
Serikali.
Pia, Wizara ya Kilimo inatoa shukrani za dhati kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Watendaji Wakuu na Wakati kayika ngazi ya Mikoa na Wilaya/Halmashauri na Maafisa Kilimo na Wagani wote kwa kazi kubwa ya kuwezesha, kuhamasisha na kusajili wakulima kwenye mfumo wa M-Kilimo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment