Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Bw. Augustino Matutu Chacha akizungumza na wasindikaji na wadau zao la mahindi wakati wa uzinduzi wa mradi maalum wenye lengo la kuchagiza wawekezaji hao katika uongezaji wa thamani wa zao hilo. Mkutano huo umefanyika katika Hotel ya Sea Scape jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa mradi huo, Bi Eunice Mbando akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Dar es Salaam
Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetoa wito kwa wakulima na wasindikaji
wa zao la mahindi kuwekeza katika teknolojia za kisasa kwa lengo la kuzuia
upotevu wa mahindi baada ya kuvunwa ili kuleta tija katika mnyororo wa thamani
wa zao hilo.
Wito
huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Bw. Augustino Matutu Chacha
wakati akizungumza na wawekezaji katika usindikaji wa zao la mahindi mara baada
ya kuzindua mradi maalum wenye lengo la kuchagiza wawekezaji hao katika
uongezaji wa thamani wa zao hilo.
“Natoa
wito kwa wasindikaji kutumia fursa za mradi huu ili kuongea tija katika
shughuli zao,” amesema.
Kwa
upande wake Msimamizi wa mradi huo, Bi Eunice Mbando amesema kuwa mfuko huo
umelenga kuwajengea uwezo wasindikaji wa ndao kuwa sehemu ya uongezaji wa
thamani wa mnyororo wa zao hilo.
“Tunaamini
Mradi huu utasaidia kuzuia upotevu wa mahindi hivyo kuleta tija kwa wakulima wa
zao hili,” amesema.
Akizungumza kwa niaba ya wasindikai walioshiriki
katika uzinduzi wa Mradi huo, Bw. Savior Chanay kutoka Kampuni ya Real World ya
mkoani Ruvuma ameishukuru Serikali kupitia TADB kwa kuja na Mradi huo ambao
utaongeza tija katika mnyororo wa thamani wa mahindi.
“Mradi huu utaleta tija katika shughuli zetu za
kila siku hivyo kuongeza uwezekano wa kuongeza kipato kwa wakulima wa mahindi,”
amesema.
0 comments:
Post a Comment