MKUU wa wilaya ya Iringa
amesema kuwa mwenge wa Uhuru unatarajia kutembelea,kuzindua,kuweka jiwe la
msingi na kukagua jumla ya miradi kumi na nne ya kimaendeleo yenye thamani ya zaidi
ya bilioni kumi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya wilaya
ya Iringa.
Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwa kwake mkuu wa wilaya hiyo Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa
mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuingia katika wilaya ya Iringa tareh 1/8/2020 ukitokea
mkoa wa Dodoma kwa lengo la kukagua miradi ya kimaendeleo katika wilaya hiyo.
Alisema kuwa mwenge wa Uhuru
unafaida kubwa kwa wananchi wa wilaya ya Iringa hivyo wananchi wanatakiwa
kujitokeza kwenye maeneo ambayo mwenge wa Uhuru utakuwa unapita kwenye miradi
au barabarani.
Alisema kuwa mwenge wa Uhuru
utarajia kutembelea katika sekta zifutazo sekta ya kilimo,shamba la mboga mboga
katika kijiji cha Kising’a,sekata ya miundombinu mwenge utaweka jiwe la msingi
katika barabara inayopita Gangilonga hadi Kihesa,kukagua mfumo wa kufundishia
wanafunzi wenye ulemavu,mradi wa maji Ismani Kilolo.
Moyo alisema kuwa ujio wa
mwenge wa Uhuru ni fursa kwa wananchi wa wilaya ya Iringa kwa kufanya biashara
mbalimbali kwenye maeneo ambaya mwenge huo utapita na kuwaongezea kukuza kipato
cha wafanyabiashara hao.
“Wananchi wa wilaya ya Iringa
changamkieni fursa ambazo zinakuja na mwenge wa Uhuru hasa kwenye biashara na
elimu kwa kupeleka bidhaa katika maeneo ambayo mwenge utapita hata mjitokeze
barabarani kuulaki mwenye wa Uhuru” alisema Moyo
Aidha katika ujio wa mwenge huo
mkuu wa wilaya hiyo,Moyo amejitolea sare za mwenge bure kwa watumishi wote wa
ofisi yake kwa lengo la kudumisha utumishi bora na kuongeza ushirikiano kazini
kwa watumishi hao.
Alisema kuwa kuna watumishi
ambao wanajitolea katika ofisi hiyo ambao hawawezi kununua sare hizo hivyo
ameamua kujitolea kuwanunulia sare hizo ili watumishi wote waweze kuhudhuria shughuli
za mwenge wa Uhuru utakapokuwa katika wilaya hiyo.
“Eee nimejitolea kwa kuwa mimi
nauwezo wa kununua sasa kuna wafanyakazi hawana uwezo huo ndio maana nimeamua
kujitolea kwa gharama zangu kuwanunulia sare hizo wafanyakazi wa ofisi hii ya
wilaya kama ambavyo ofisi nyingine zimefanya”alisema Moyo
Kwa upande wao baadhi ya
wafanyakazi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Iringa,walisema kuwa wanashukuru kwa
sare hizo ambazo zitachangia kuongezeka kwa ushirikiano baina ya watumishi wa
ofisi hiyo na mkuu wa wilaya hiyo.
Walisema jambo alilolifanya mkuu wa wilaya ni kuongeza hali ya kuwafanya wafanyakazi kuongeza bidii ya kufanya ya kwa kuwatumikia wananchi ambao ndio jukumu la namba moja kwenye utumishi wao serikalini.
0 comments:
Post a Comment