wachezaji wa Timu ya Iringa All Stars Veterens wakishangilia ubingwa mbele ya kiungo wa timu ya Iringa Veterans.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Timu ya Iringa All Stars Veterans imeibuka bingwa wa Bonanza la Iringa Combine Veterani kwa kuifunga timu ya Iringa Veterans kwa goli moja bila katika uwanja wa kumbukumbu ya Samora lililokuwa limeshirikisha jumla timu sita za veteran mkoani Iringa.
Timu ya Iringa All Stars Veterans ilianza kwa kuifunga timu ya Ruaha stars Veteran kwa jumla ya magoli mawili kwa bila(2-0) na mchezo wa pili ulikuwa kati ya Timu ya Iringa All Stars Veterans na Ilula Veteran na timu ya Timu ya Iringa All Stars Veterans ilibuka na ushindi wa goli nne kwa bila (4-0) na kuipeleka timu hiyo moja kwa moja katika hatua ya fainali.
Katika hatua ya fainali ya Bonanza la Iringa Combine Veterani timu ya Iringa All Stars Veterans imeibuka bingwa wa Bonanza la Iringa Combine Veterani kwa kuifunga timu ya Iringa Veterans goli moja kwa bila(1-0), goli lililofungwa na kiungo machachali wa wa timu hiyo anayejulikana kwa jina la Omary Albert aliyeingia kipindi cha pili akitokea bench kuchukua nafasi ya Ramadhan Shemuhilu.
Katika bonanza hilo timu ya Iringa All Stars veterans iliibuka bingwa katika idara zote kwa kumtoa mfungaji bora wa bonanza hilo Ramadhan Shemuhilu kwa kufunga jumla ya magoli matatu huku akifuatiwa na Omary Albert aliyefunga magoli mawili,kwa upande wa mchezaji bora wa bonanza hilo, timu ya Iringa All Stars veterans ilitoa tena mchezaji bora wa bonanza hilo anayejukana kwa jina Steve Lihawa maarufu (Iniesta).
Katika bonanza hilo timu ya Iringa All Stars Veterans ilikuwa timu iliyokuwa inamvuto kwa kupiga pasi nyingi kwa uelewano maarufu kama kampa kampa tena jambo ambalo liliwafanya mashabiki na baadhi ya wachezaji wa timu nyingine kuvutiwa na kiwango cha timu hiyo.
Hata hiyo haikuwa kazi rahisi kushinda ubingwa huo kwa kuwa timu kama Mafinga Veteran,Iringa Veterani na Ruaha stars veteran walikuwa wanawachezaji ambao kwa kiasi kikubwa walionyesha kandada safi uwanjani.
Kwenye mchezo wa fainali baina ya timu ya Iringa All Stars Veterans Na Iringa Veteran kulikuwa na ushindani katika eneo la kiungo ambalo kwa timu ya Iringa All Stars Veterans walikuwa na viungo watatu ambao ni Ally Msigwa,Winfredy Fyataga na Steve Lihawa na baadae aliongezeka Ally Luambano kiasi kwamba walifanyikiwa kukivuruga kiungo cha timu ya Iringa Veteran kilichokuwa chini ya Alex Mbewe na wenzake.
Wakizungumzia bonanza hilo
baadhi ya wachezaji walioshiri waliwapongeza timu ya Iringa All Stars Veterans kwa
kuwa mabingwa na kutoa sifa kede kede kwa waandaji wa bonanza hilo ambalo
lilikuwa kubwa na liliwavutia watu wengi
Naye kepteni wa timu ya Iringa All Stars Veterans Lissa Mwalupindu alisema kuwa wamelitumia bonanza hilo kwa ajili ya kujiandaa na bonanza la kitambi Noma litakalofanyika mwishoni wa wiki hii jijini Arusha
Kwa upande wake Katibu mkuu wa umoja wa veteran mkoa wa Iringa na mratibu wa bonanza hilo Pastory Kwambiana alisema kuwa lengo la bonanza hilo ni kuleta umoja na mshikamano kwa wachezaji wa zamani na kuwa kitu kimoja katika kukuza na kuinua soka la mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa umoja wa maveteran mkoa wa Iringa umedhamilia kuona heshima ya soka inarudi mkoani Iringa kwani wamepanga kuwa na utaratibu wa kuvitembelea vilabu ili kubadilishana mawazo yatakayoisaidia timu.
Bonanza la Iringa Combine Veterani, limeshirikisha timu sita ambazo ni Iringa veterans, Mkwawa veterans, Ruaha veterans, Mafinga Veterans Ilula veterans na Iringa All Stars Veterans
0 comments:
Post a Comment