Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema Nchi ya Brazil ipo tayari kushirikianana kitaalamu na Tanzania katika kukuza Mchezo wa Soka Nchini pamoja na Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya iliyopo Jijini Mwanza kwakufanya Programu ya kubadilishana Wakufunzi wa michezo.
Mhe Bashungwa amesema hayo Mei 21, 2021Jijini Dar es Salaam alipokutana na Balozi wa nchi hiyo Mhe. Antonio Augusto Martins Cesar ambapo amemuomba Mhe. Balozi huyo kuialika timu ya Taifa ya Wanawake ya nchi hiyo kuja kucheza na Timu ya Taifa ya Wanawake ya hapa nchini ili kuleta Motisha ya kukuza Michezo ya wanawake ikiwa ni sehemu ya kutimiza Maagizo aliyoyatoa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni Bungeni Jijini Dodoma.
Naye Balozi huyo amemshukuru Waziri Mhe. Bashungwa kwa kupata muda wa kuonana nae ambapo amepokea maombi ya ushirikiano baina ya Brazil na Tanzania Katika sekta ya Michezo na Kuahidi kuwasiliana na Serikali yake mapema iwezekanavyo ili kujua ni jinsi gani wanaweza kufanya mabadilishano ya wakufunzi wa michezo na pia kukaa na Idara ya Michezo kuainisha ni namna gani wanaweza kukisaidia Chuo cha Maendeleo ya Michezo Nchini.
Aidha , Balozi huyo ameridhia kuialika timu ya Taifa ya Wanawake ya nakuahidi kulifayia kazi suala hilo.
0 comments:
Post a Comment