Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega akiongea na wachezaji na wananchi waliofika Uwanja wa Ushirika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro kwenye Mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika leo Februari 28, 2021. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Rajabu Kundya na shoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Irene Mtiganzi.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega akimvalisha medali mshindi wa kwanza wa km 42 Augustino Sule aliyekimbia kwa 2:18:04 wakati wa Mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika leo Februari 28, 2021U uwanja wa Ushirika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega (kushoto) akiongea na Filbert Bayi mara baada ya kumaliza kukimbia km tano wakati wa Mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika leo Februari 28, 2021U uwanja wa Ushirika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Lucas Mhavile maarufu kama Joti (katikati) wakati wa Mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika leo Februari 28, 2021U wanja wa Ushirika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Yusuph Singo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega (wa tano kulia waliosimama) akiwa katika picha ya pamoja nwashindi wa km 21 mara baada ya kutoa zawadi kwa washindi hao wakati wa Mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika leo Februari 28, 2021U wanja wa Ushirika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuangalia Mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika leo Februari 28, 2021U wanja wa Ushirika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Na Eleuteri Mangi, WHUSM-Moshi
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega amewataka waandaaji wa Mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon wawe wabunifu na kuongeza vionjo vipya kwenye mashindano hayo ili kuwavutia watu wengi zaidi kuja kushiriki mashindano na kuja kujionea vivutio vizuri vilivyopo katika mkoa wa Kilimanjaro na taifa kwa kwa ujumla.
Naibu Waziri Ulega amesema hayo leo Februari 28, 2021 alipokuwa akifunga Mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika Uwanja wa Ushirika Manispaa ya Moshi.
“Ninyi kama wataalamau wenye uzoefu angalieni na muongeze ubunifu ili kuboresha mashindano haya, wanapokuja watu hapa uchumi uendelee kukua zaidi ambapo wajasiriamali waendee kupata pesa zaidi na wenye kuuza baishara ndgondogo waendendelee kupata pesa zaidi tujenge uchumi wetu” amesema Naibu Waziri Ulega.
Pia amewataka waandaaji wa mashindano hayo hayarudi nyuma yanasonga mbele na yawe na ubunifu na yaweze kutangazika zaidi duniani kote ili kuwavuta wakimbiaji wengi wenye majina makubwa duniani waje kushiriki mashinfdano hayo.
Aidha, Naibu Waziri Ulega amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaonesha Watazania namna nzuri ya kuiwekezaji na fursa za kibiashara katika taifa letu bado zipo wazi ambapo maboresho hayo yakifanyika yatawavuta wawekezaji wengi zaidi waje kuwekeza nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Moshi Rajabu Kundya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Anna Mughwira ameishukuru Serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya michezo nchini ambapo amesema mashindano hayo yamekuwa chachu ya kuwakutanisha wananchi kutoka mikoa mingine na mataifa mbalimbali kwa kuwa zimeshiriki zaidi ya nchi 55.
Wataalamu wa afya wametuhakikishia akili safi daima hukaa kwenye mwili safi, na mwili safi ni ule ambao haujachokonolewa na maradhi na namna pekee ya kuulinda mwili ni kufanya mazoezi na kulinda afya ya mwili na akili, hii ilikuwa ni fursa muhimu ambapo amewasihi Watanzania tuendelee kufanya mazoezi kujiandaa na mashindano yajayo.
Naye Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Irene Mtiganzi ambao ni moja ya wa dhamini ya mashindano amesema kampuni yao inajivunia kuwa na mchango katika kukuza utalii wa michezo nchini hatua inayosaidia kuongeza watalii wa ndani nan je ya nchi katika viutio mbalimbali vilivyopo katika mkuo huo.
Mshindi wa kwanza katika mbio za km 42 kwa wanaume na wanawake amepata zawadi ya Shilingi milioni 4,100,000 kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo na kuongezewa kiasi cha Shilingi 1,500,00 ikiwa motisha kwa Watanzania waliofanya vizuri kwenye mashindano hayo na kufanya jumla ya fedha walizopokea jkufikia kiasi cha Shilingi 5,600,000.
Mashindano ya Kilimanjaro marathon ya mwaka huu ni ya 19 kufanyika tangu kuanzishwa kwake 2003 ambayo yameshirikisha wachezaji zaidi ya elfu 12 kutoka nchi zaidi ya 55 ambapo Watanzania wamefanya vizuri katika mbio za km 42 kuanzia mshindi wa kwanza ambaye ni Augustino Sule aliyekimbia kwa 2:18:04 kwa upande wa wanaume huku kwa upande wa wananwake Watanzania wameongoza kuanzia mshindi wa kwanza ambaye ni Jackline Sakilu aliyekimbia kwa 02:45:44 hadi nafasi ya tisa wakati nafasi ya 10 imechukuliwa na Dominic Kremer raia kutoka nchini Netherland.
0 comments:
Post a Comment