Salamu za Waziri Mhe. Innocent Bashungwa wakati wa Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Jijini Dar es Salam.
Ziara hiyo iliyofanyika Februari 25, 2021 Jijini Da es Salaam ilikua na lengo la kuzindua Jengo la Jitegemee House lenye Studio za Channel Ten, Channel Ten Plus, Redio Magic FM na Classic FM pamoja na Soko la Kisutu.
Katika ziara hiyo Waziri Mhe. Bashungwa amekishukuru Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwekeza katika tasnia ya Habari ambayo ni sekta inayosaidia wananchi kupata habari za ukweli na uhakika kuhusu utekelezaji wa Serikali kwa wananchi wake.
"Nitumie fursa hii kukaribisha Chama cha Mapinduzi kwenye tasnia ya michezo na Sanaa kama mlivyowekeza kwenye tasnia ya habari, ipo pia fursa kubwa ya kuwekeza kwenye michezo kwani tuna viwanja vya michezo vingi sehemu mbalimbali hapa nchini, wawekezaji wagonge hodi kwenye Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Ikiwezekana tutumie 'PPP-Public Private Patnership' (Ubia kati ya Serikali na Mashirika Binafsi) kuwekeza kwenye viwanja ili visaidie kwenye soka na sanaa kwa ujumla," alisema Mhe. Bashungwa.
0 comments:
Post a Comment