Na Joyce Kasiki,Dodoma.
MGANGA Mkuu wa Jiji la Dodoma Gatete Mahava amewapongeza waandishi wa habari kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuelimisha jamii katika mambo mbalimbali hasa katika kipindi cha maambukizi ya virus vya Corona vilivyosababisha homa Kali ya mapafu .kwa kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa huo.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu Dkt.Mahava amesema uelimishaji huo ulisaidia wananchi kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo yakiwemo makundi maalum ya akina mama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Amesema kutokana na hofu iliyokuwepo kipindi hicho akina mama wengi wajawazito walihofia kwenda kliniki na kushindwa kuwapeleka watoto wao kupima uzito na kupata chanjo mbalimbali kwa kuhofia kuambukizwa virus vya ugonjwa huo.
"Hii ilikuwa ni hatari maana mama mjamzito ni lazima ahudhurie kliniki kwa.ajili ya kuangaliwa Afya yake pamoja na mtoto aliye tumboni,lakini pia mtoto mdogo anatakiwa ahudhurie kliniki kwa ajili ya kupatiwa chanjo na kuangaliwa maendeleo ya Afya yake" alisema Dkt.Mahava na kuongeza kuwa.
"Sasa ilifika hatua akina mama hawa waliogopa kuhudhuria kliniki lakini kwa jinsi waandishi wa habari walivyoshiriki mapambano yale hasa katika eneo la Afya ya mama na mtoto,na Rais John Magufuli kuingilia kati kuwatoa wananchi hofu kuhusu ugonjwa huo idadi ya mahudhirio ya kliniki kwa.makundi hayo yaliongezeka."
Vilevile amesema mbali na mahudhurio ya kliniki ya mama na mtoto kuongezeka pia idadi ya wagonjwa waliofika katika zahanati na vituo vya Afya vya jijini humo iliongezeka .
Dkt.Mahava ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi jijini humo waendelee kuchukua tahadhari hasa kwa kunawa mikono kila wakati ili kusaidia kujikinga na magonjwa ya mlipuko huku akisema kwa kipindi kile magonjwa ya matumbo na kuhara yalipungua.
"Wakati tunajikinga na Corona ilisaidia sana kupunguza magonjwa yanayotokana na uchafu kama homa ya matumbo na kuhara."
0 comments:
Post a Comment