METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, December 10, 2020

BASHUNGWA NA ULEGA WAFIKA OFISINI NA KUANZA KAZI RASMI MUDA MCHACHE BAADA YA KUAPISHWA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Innocent Lugha Bashungwa (wapili kushoto) akiwa katika picha na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto), Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Abdallah Hamis Ulega (wapili kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Ally Possi (kulia) baada ya kuwasili ofisini Mji wa kiserikali Mtumba Dodoma muda mchache baada ya kuapishwa katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Leo tarehe 09 Desemba 2020.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Innocent Lugha Bashungwa (waliokaa wapili kushoto) akiwa katika picha na viongozi na wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo baada ya kupokelewa ofisini Mji wa kiserikali Mtumba Dodoma muda   mchache baada ya kuapishwa katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, (waliokaa kushoto) ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi, (waliokaa wapili kulia) ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Abdallah Hamis Ulega na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Ally Possi (waliokaa kulia). Leo tarehe 09 Desemba 2020.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Innocent Lugha Bashungwa akisaini kitabu kwa ajili ya kuanza kazi rasmi alipowasili Ofisini kwake Mji wa kiserikali Mtumba Dodoma muda mchache baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Leo tarehe 09 Desemba 2020.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akiwakaribisha na kuwatambulisha kwa watumishi na wafanyakazi wa wizara hiyo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Innocent Lugha Bashungwa (katikati) na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Abdallah Hamis Ulega (kulia) baada ya kuwasili ofisini Mji wa kiserikali Mtumba Dodoma muda mchache baada ya kuapishwa katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Leo tarehe 09 Desemba 2020.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Innocent Lugha Bashungwa akiongea na watumishi na wafanyakazi wa wizara ya ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika kikao cha kuwakaribisha yeye na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Abdallah Hamis Ulega) baada ya kuwasili ofisini Mji wa kiserikali Mtumba Dodoma muda mchache baada ya kuapishwa katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Leo tarehe 09 Desemba 2020. (Picha na Eliud Rwechungura).

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com