Na
Fredy Mgunda,Iringa
Watumishi wa Shamba la Miti Sao Hill wanapewa mafunzo ya mfumo wa wazi wa mapitio ya utendaji kazi ambayo yanalenga kuwakumbusha watumishi juu ya ujazaji wa fomu hizo ili kufikia malengo ya taasisi.
Mafunzo haya yanawakumbusha watumishi pia juu ya upangaji wa wa malengo ,utekelezaji, ufuatiliaji na mapitio ya utendaji kazi ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Akiwapa mafunzo hayo Mkufunzi wa mafunzo hayo Frank Kamugisha aliwataka watumishi kutumia mafunzo haya kama sehemu ya kujikumbusha na hivyo kuhakikisha mafunzo haya yanaendelea kuwasaidia katika kufikia malengo ya taasisi.
Naye Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti Sao Hilll Juma Mwita Mseti aliwaasa watumishi kuelewa mada zote zitakazotolewa ili kuhakikisha kunakuwa na uelewa wa pamoja katika kuhakikisha malengo yanayoweka kufikiwa kwa wakati na hatimaye kufikia malengo ya taasisi nzima.
Kwa upande wake Afisa utumishi wa shamba hilo Felista Bayo alisema kuwa mafunzo haya ni muhimu kwani yanatasadia katika utendaji wa kazi wa kila siku na hivyo kufanya kila mtumishi kuwajibika katik nafasi yake kulingana na malengo yaliyowekwa.
Lakini pia afisa habari Mwanaisha Luhaga alisema kuwa Mafunzo hayo yanawasaidia kuwakumbusha wajibu wao katika kazi wanazozifanya za kila siku kwani bila kuwa na malengo hawawezi kuwa na utekelezaji wenye tija.
“Hapa tunafundishwa jinsi ya kuweka malengo, utekelezaji ,ufuatiliaji na mapitio ya utendaji kazi.Hii inasaidia sana kufikia malengo ya taasisi kwani tuna uhakika kila mmoja atatimiza wajibu wake na kwa wakati” Luhanga
Mafunzo hayo yanatolewa na Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana TFS ambayo yatafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 16 Novemba 2020.
0 comments:
Post a Comment