
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akionesha Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais alichokabidhiwa na
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage
mara baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu
uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.
Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipokea Cheti cha
Ushindi wa Kiti cha Makamu wa Rais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage mara baada ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kutangazwa mshindi
kwa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu
uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akizungumza na Wageni mbalimbali waliofika katika hafla fupi ya
kukabidhiwa Cheti cha Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akimpongeza Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mara baada
ya kukabidhiwa Cheti cha Ushindi kwa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Waliogombea Urais kupitia vyama Mbalimbali vya Upinzani nchini wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa katika hafla fupi ya kukabidhi Cheti cha Ushindi kwa Kiti cha Urais zilizofanyika katika Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma leo tarehe 01 Novemba 2020.
0 comments:
Post a Comment