Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Suyuph Singo akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu mashindano ya NBC Marathon yatakayofanyika Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Kushoto ni Meneja Mahusiano na Serikali wa Benki ya NBC Bw. William Kallaghe.
Meneja Mahusiano na Serikali wa Benki ya NBC Bw. William Kallaghe akieleza kwa
waandishi wa habari kuhusu mwitikio wa wananchi kushiriki katika mashindano ya
NBC Marathon yatakayofanyika Jijini Dodoma Novemba 22, 2020 .
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa
kuwa Mgeni rasmi katika mashindano ya NBC Marathon yatakayofanyika Novemba 22,
2020 Jijini Dodoma ambapo pia atashiri mbio za Kilomita 5.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Suyuph Singo
kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo leo Novemba 21, 2020 Jijini
Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kueleza hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya
mashindano hayo.
“Lengo
la mashindano ya NBC Marathon ni kwa ajili ya kuchangisha fedha kusaidia
mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kansa ya shingo ya kizazi katika hospitali
ya Ocean Road ya jijini Dar es salaam” alisema Bw.Singo.
Mashindano
hayo yatashirikisha wanariadha 3000 ambao wanaendelea kujisajili kwa njia ya
mfumo wa kielektroniki na watakimbia mbio za kilomita 5, 10, 21 na 42 ambapo
jumla ya sh. Milioni 45.4 zitatolewa kama zawadiwa kwa washindi wa mbio hizo.
Kwa
upande wake, Meneja Mahusiano na Serikali wa Benki ya NBC Bw. William Kallaghe
amesema kuwa maandalizi ya mbio hizo yamekamilika na njia zote zitakazotumika
kwa mashindano hayo zimetambuliwa na kuthibitishwa na Shirikisho la Riadha
Duniani kwa kukidhi vigezo na tayari
wamepewa cheti cha kutambuliwa na Shirikisho hilo.
“NBC
ipo makini na mashindano haya na imeingia mkataba wa miaka mitano kudhamini
mashindano haya ambapo mapato yake yanatokana na usajili wa wanaridha ambao ada
yao ya usajili ni Sh. 25,000/= zote zitaelekezwa hospitali ya Ocean Road
kuwahudumia wagonjwa wanasumbuliwa na tatizo la kansa ya shingo ya kizazi”
alisema Bw. Kallaghe.
Aidha, amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha pia wanariadha kutoka nchi tatu ambazo ni Kenya, Malawi na Uganda ambapo washiriki 35 watashiriki na wote wamefanyiwa vipimo vya Covid-19 na hawana tatizo lolote.
0 comments:
Post a Comment