Kampuni Sita
zinazozalisha Saruji na Moja inayozalisha Mbolea yamekutana na kujadili na Serikali kuhusu tozo mbalimbali za Usafirishaji (Clearance fee) na tozo za
Ukaguzi (Inspection fee).
Lengo la kukutana na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, ni kujadili
na kupitia (Review) tozo ya usafirishaji (Clearance fee) na
tozo ya Ukaguzi (Inspection fee). Wamesema tozo ya usafirishaji
inatozwa na wizara mbalibali kama vile Madini, Kilimo na Viwanda na Biasha
kiasi kwamba inakuwa kero na kuiomba Wizara ya Madini, tozo hiyo ielekezwe
kwenye wizara moja, huku tozo la Ukaguzi ifutwe ama ipunguzwe.
Mjadala huo umefanyika
Octoba 7, 2020 Jiji Dodoma ukiwahusisha wataalam mbalimba akiwemo Kamishna wa
Madini Mhandisi David Mulabwa, Makamishna Wasaidizi wa Madani, Maafisa
mbalimbali wa Tume ya Madini na Maafisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
Akizungumzia Prof.
Msanjila kuhusu malipo ya tozo kufutwa au kupunguza, alisema, Serikali
haiwezi kuziondoa kwa sababu zimepangwa kwa mujibu wa sheria na zilijadiliwa
kwa mapana na wadau mbalibali na kufiki maamuzi hayo. Ameongeza kuwa
mabadiliko haya yanahitaji mjadala mkubwa na wadau wengi.
Ameongeza kuwa, jambo
la kujadili ni suala la kutotwa tozo ya aina moja kwa wizara kadhaa, alisema
atalishugulikia na atakaa na Makatibu Wakuu wenzake wa wizara husika kuona
namna ya kulitatua ili kuondoa kero hiyo. “Andikeni kwa maandishi mniletee
muanishe hizo kero na mimi nitawaita Makatibu wenzangu tutakaa na kujadili,”
alisema Prof.Msanjila. Serikali inahitaji Wawekezaji na Wawekezajizi waisaidie
Serikali ili iweze kutoa huduma kwa Wananchi hivyo kulipa tozo ni muhimu sana.
Mmoja kutoka kwa
Kampuni hizo, ambae ni Mwanasheria Mkuu wa Kampuni ya Mbeya Cement, Emmanuel
Salla, alisema maombi yao yalilenga kujadili na kuptia (Review) tozo za
usafirishaji na tozo ya ukaguzi ili wao waweze kupunguza bei ya bidhaa
inayokwenda kwa wananchi.
Mkuu wa Idara ya Fedha
wa Kampuni ya Tanga Cement, Isaac Lupokela, alisema, “Tumekuwa na mkutano wenye
tija ambao umefungua wigo mpana katika kuhakikisha maendeleo ya Viwanda na
Serikali. Pongezi kwa Serikali kwa kuwa supportive sana. Ni
mabadiliko makubwa katika taifa tumeyaona na tunapongeza,” alisema Lupokea.
Miongoni mwa Kampuni zinazozalisha Saruji na Mbolea ni; Dangote, Twiga Cement, Tanga Cement, Mbeya Cement, Lake Cement, Maweni Limstone, na Minjingu.
0 comments:
Post a Comment