METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, September 14, 2020

WANANCHI MSIBABAISHWE CHAGUENI CCM CHAMA CHENYE AJENDA YA MAENDELEO - HASUNGA

Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Japhet Hasunga akionyesha ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2020/2025 wakati wa mkutano ya kampeni katika Mtaa wa Old Vwawa Kata ya Vwawa leo Tarehe 14 Septemba 2020.

Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa mkutano ya kampeni katika Mtaa wa Old Vwawa Kata ya Vwawa leo Tarehe 14 Septemba 2020.

Dehemu ya viongozi wa CCM wakifatilia mkutano wa Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Japhet Hasunga wakati wa mkutano ya kampeni katika Mtaa wa Old Vwawa Kata ya Vwawa leo Tarehe 14 Septemba 2020.


Sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano wa Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Japhet Hasunga wakati wa mkutano ya kampeni katika Mtaa wa Old Vwawa Kata ya Vwawa leo Tarehe 14 Septemba 2020.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akiwa katika mikutano ya kampeni katika Mtaa wa Old Vwawa, Senya na Ilembo Kata ya Vwawa amewaeleza wananchi mambo manne ya muhimu ambayo yamefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika kipindi cha muda mfupi tangu aingie madarakani Octoba 2015.

Mambo hayo muhimu aliyowaeleza wananchi ni pamoja na Ujenzi wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme katika Mto Rufiji.

Alisema kuwa Mradi huo unajengwa kwa fedha za ndani upo katika eneo la Selous ambalo ni moja ya maeneo ya turathi za dunia, Mradi huo ambao unafahamika pia kwa jina la Stieglers Gorge, unatazamiwa kuzalisha zaidi ya megawati 2,000 za umeme, hatua ambayo ameeleza kwamba itasaidia kupunguza tatizo la nishati hiyo muhimu kiuchumi na kijamii. Hivyo Tanzania kuwa na utoshelevu wa umeme.

Hasunga ameeleza pia kuhusu Ujenzi wa reli ya kisasa, ambapo alisema kuwa nchi nyingi zilizoendelea duniani zinatumia reli kuchochea ukuaji uchumi na biashara kwa sababu usafirishaji kwa kutumia njia hiyo una uwezo wa kubeba mizigo mikubwa kwa mara moja na kwa gharama nafuu kulinganisha na aina nyingine za usafirishaji.

Alisema, Serikali imedhamiria kujenga Reli ya Kisasa (SGR) kwa kiwango cha kimataifa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) ndilo limepewa dhamana ya kusimamia mradi huo. Reli inayojengwa (Standard Gauge), yenye upana wa mita 1,435 ndio mfumo unaotumika sasa ukikadiriwa kuchukua asilimia 50 ya mitandao ya reli duniani.

Katika mikutano yake ya kampeni ambayo imeungwa mkono na mamia ya wananchi anayoifanya katika Jimbo hilo kwa takribani,  Hasunga ametaja pia juhudi za Rais Magufuli kwa kuamua kununua Ndege zaidi ya nane.

Alisema, kuwa Miaka ya nyuma Kabla ya Rais wa Tanzania aliyopo sasa madarakani Dkt John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais, Shirika la ndege nchini Air Tanzania lililoanzishwa tangu Mwaka 1977 lilikuwa na Ndege moja aina ya Bombardier DASH8 Q300 ambayo ilikuwa ikihudumu tangu 2011. Baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani Mwaka 2015 na kuanza mkakati wa kulifufua Shirika hilo na kuonesha nia ya kununua ndege mpya za Tanzania.

Kuna Bombardier DASH8 Q400 tatu, mbili ambazo zilifika Tanzania Septemba 2016 na moja Juni 2017; Bombardier CS300 mbili na Boeing 787 Dreamliner ambazo zilitua Tanzania kati ya mei na Julai 2018. Ndege nyingine ni Airbus A220-300.

Hasunga alisema ununuzi wa ndege hizo ni mkakati muhimu wa serikali inayotekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ambayo ni sehemu ya kurahisisha usafirishaji wa mazao ya Kilimo hivyo kuboresha sekta ya Kilimo sambamba na kuinua kipato cha wananchi kwani mazao mengi yanaoza shambani lakini kupitia usafirishaji huo mazao yote yatakuwa na tija.

Jambo la nne ni kuhusu Elimu bure, Hasunga alisema kuwa Katika kipindi cha muda mrefu Tanzania kulikuwa na wimbi la wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo kutokana na wazazi/walezi kukosa fedha za kuwalipia ada. Katika kuliona hilo Rais Magufuli aliamua kufuta ada kuanzia elimu ya awali hadi sekondari, jambo ambalo limeongeza idadi ya wanafunzi ambao wamejitokeza kusoma.

Alisema kuwa maono ya Rais Magufuli yamezaa matunda kwani wananchi wengi sasa watoto wao wananufaika na serikali yao kwani imekuwa mkombozi katika sekta ya elimu.

Hasunga amewatakla wananchi katika Mkoa wa Songwe na Tanzania kwa ujumla wake kujitokeza kwa wingi Octoba 28, 2020 na kumpigia kura Rais Magufuli, Wabunge na Madiwani wote wa CCM ili kuendeleza maendeleo endelevu yaliyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2020/2025.

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com