Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw Gerald Kusaya akikagua
mifuko maalumu ya kuhifadhia nafaka unaomwezesha mkulima kuhifadhi nafaka kwa
muda mrefu bila kuharibika. (Picha zote na Innocent Natai)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw Gerald Kusaya,akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa Taasisi ya TPRI,Taasisi inayojishughulisha na utafiti wa Vuatilifu na visumbufu vya mimea na mazingira.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw Gerald Kusaya,akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa Taasisi ya TPRI,Taasisi inayojishughulisha na utafiti wa Vuatilifu na visumbufu vya mimea na mazingira.
Na Innocent Natai, TPRI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw Gerald Kusaya amezitaka Taasisi
zilizopo chini ya Kilimo zinazoshiriki maonesho ya nane nane kuhakikisha
teknolojia wanazozionyesha katika maonesho hayo zinawafikia wakulima kwa
wakati,
Hii ni ili kuwasaidia kuondokana na Kilimo cha kubahatisha au cha
mazoea,Ameyasema hayo alipokuwa akitembelea mabanda ya Taasisi hizo katika
maonesho hayo yaliyozinduliwa mapema hivi leo Bariadi mkoani Simiyu
Kusaya amesema upo umuhimu wa kuwapa elimu na teknolojia mpya
wakulima kwani wamekuwa wakilima Kilimo kisicho na tija angali kunataasisi za
utafiti zinazozalisha teknolojia bora zitakazo weza kuwasaidia wakulima
kuondokana na aina hiyo ya kilimo
Ameongeza kuwa Kilimo sasa kimekuwa tena sio cha watu wasio na na
elimu au wasio na ajira bali kimekuwa ndio mhimili mkuu wa taifa hasa katika
kipindi hichi Taifa linapoelekea katiaka uchumi wa viwanda kwani viwanda
vinategemea malghafi kutoka katika kilimo
Kusaya ameongeza kuwa dhumuni la maonesho hayo kufanyika kila mara
sio tu kuonyesha na kushiriki bali ni kuhakikisha kazi zinazofanywa na Taasisi
hizo za Kilimo,Mifugo na Uvuvi zinaonyeshwa na kuwafikia wakulima eidha kwa
elimu au vifaa
pia Bw Kusaya ameitaka Taasisi ya TPRI kuendelea kudhibiti
Viuatilifu visivyo kidhi vigezo kuingia au kutumiaka hapa nchini kwani vimekuwa
ndio sababu nyingine ya wakulima wengi kupata hasara katika Kilimo na hatimae
kukimbia katika tasnia ya Kilimo
Aidha pia ameutaka uongozi wa Tume ya Vyuo Vikuu vya Kilimo
kuhakikisha wanatoa elimu kwa vitendo kwa wanafunzi ili kuhakikisha
wanapomaliza elimu zao wanakwenda vijijini kuwasaidia wakulima
Maonesha hayo ya nane nane yamezinduliwa hivi leo kitaifa hapa
Bariadi Mkoani Simiyu,mgeni rasmi akiwa ni Makamu wa Rais Mhe Samia Suluh
Hassan na yanatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 8/8/2020 Ambapo ndio siku ya
kilele mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment