Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama akizungumza wakati wa mkutano baina yake na wanawake viongozi wa
vyama vya siasa nchini ulioambatana na hafla ya kumpongeza kwa namna
alivyoongoza na kuimarisha vyama vya siasa kwa
kuhakikisha kumekuwa umoja na
mshikamano leo jijni Dodoma tarehe 13
Julai 2020. Kulia ni Msajili wa Vyama
vya Siasa, Jaji Francis Mutungi na kushoto ni Mratibu wa umoja huo ambaye pia
ni Katibu Mkuu wa UDP, Bibi. Saumu Rashid.
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji
Francis Mtungi akizungumza wakati wa mkutano wa umoja wa wanawake viongozi wa
vyama vya siasa uliombatana na hafla ya utoaji tuzo ya pongezi na shukrani kwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama(katikati) kwa namna
alivyoongoza na kuimarisha vyama vya siasa kwa
kuhakikisha kumekuwa umoja na
mshikamano leo jijini Dodoma. Kushoto ni Mratibu wa umoja huo ambaye pia ni
Katibu Mkuu wa UDP, Bibi. Saumu Rashid.
Kiongozi
wa Viongozi Wanawake wa Vyama vya Siasa, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha
UDP Bi.Saumu Rashid akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake kabla ya
kukabidhi zawadi pamoja na tuzo Waziri Mhagama kwa kutambua utendaji kazi wake
hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu,Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama amewaasa wanawake kutokubali kutumiwa na vyama vya siasa kama mawakala
Waziri Mhagama ametoa wito huo leo
jijini Dodoma wakati akizungumza na umoja wa wanawake viongozi wa vyama vya
siasa nchini katika mkutano baina yake na viongozi hao uliombatana na hafla ya
kumpongeza kwa namna alivyoongoza na kuimarisha vyama vya siasa kwa kuhakikisha kumekuwa umoja na mshikamano.
Mhe.Mhagama amekutana na Viongozi
wanawake kwa lengo la kumpongeza kwa kusimamia vema vyama vya siasa ambapo
wizara yake ndio inayohusika na usimamizi wa vyama vya siasa kupitia Ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Waziri Mhagama amesema wanawake wana
nguvu kubwa na uwezo wa kuwa viongozi na ndio maana Rais Dk John Magufuli
amewaamini katika nafasi mbalimbali na hata wakati alipoteuliwa na chama chake
kuwa mgombea Urais wa CCM alimchagua tena Mama Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea
mwenza wake kwa mara pili.
” Nguvu yetu wanawake ni kubwa sana na
kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi nitoe rai kwenu kugombea nafasi za
Uongozi kupitia vyama vyenu, chukueni fomu mkachuane kwenye majimbo na kata
msiogope kwa sababu uwezo tunao”amesisitiza
Tusikubali kusubiri nafasi za upendeleo
kama tuna lengo la kufikia 50/50 basi inatulazimu pia tuingie kwenye uwanja wa
mapambano ili tupime nguvu zetu, na kwa sababu sisi tuna uwezo mkubwa basi
naamini tutashinda,” Amesema Mhagama.
Kwa upande wake Msajili wa Vyama vya
Siasa Jaji Francis Mtungi amemshukuru Waziri Mhagama kwa uvumlilivu alionao
hali iliyosaidia katika kuratibu zoezi zima la kuimarisha umoja na mshikamano
miongoni mwa wanasiasa bila kujali itikadi za vyama vyao.
Aidha Jaji Mutungi amewataka viongozi
hao kutoruhusu kuwa sehemu ya machafuko yanayosababishwa na baadhi ya wanasiasa
wasio na uzalendo wa Nchi yao.
Akizungumzia hoja aliyoitoa Mhe. Rais
yakuwa kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki, Jaji Mutungi ameongeza kuwa siyo
tukwamba uchaguzi utakuwa huru na wa haki unapaswa kumalizika kwa Amani pia
kama ambavyo imekuwa desturi ya nchi yetu hivyo amewataka wanawake hao viongozi
kuwa chachu ya kusimamia Amani na utulivu wtunapoelekea katika Uchaguzi Mkuu
katika maeneo yao.
” Niwapongeze kwa Umoja wenu huu kama
viongozi wanawake, mmekuja hapa pamoja mkiwa mmevaliwa sare moja ambayo siyo ya
vyama vyenu, niwasihi Umoja huu huu ndio muende nao kwenye uchaguzi mkiweka
mbele maslahi ya Nchi yetu,” Amesema Jaji Mutungi.
Awali
Mratibu wa wanawake viongozi wa vyama
ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha UDP,Bi. Saumu Rashid amemshukuru
Waziri Mhagama kwa kukubali kupokea zawadi yao na kumpongeza kwa namna ambavyo
amevilea vyama vya siasa kwa muda wote wa miaka mitano.
” Tunakupongeza sana Waziri kwa
ushirikiano mkubwa ambao umetupatia, hakika umekua mwema kwetu na tunakuombea
urudi bungeni, sisi kama viongozi wanawake tunakuahidi tutakua mstari wa mbele
kuchochea amani na utulivu kwenye uchaguzi mkuu,” Amesema Saumu.
0 comments:
Post a Comment