Mkurugenzi wa Shirika la Kuhudumia watoto SOS Childrens Village Tanzani David Mlongo akiwa kwenye shamba la nyanya la wanawake wajane wilayani Mufindi mkoani Iringa
Mkurugenzi wa Shirika la Kuhudumia watoto SOS Childrens Village Tanzani David Mlongo akiwa kwenye shamba la nyanya la wanawake wajane wilayani Mufindi mkoani Iringa
Wanawake wa kikundi cha akina mama Wajane cha kijiji cha Iyela wakiwa kwenye shamba la nyanya
FREDY MGUNDA,MUFINDI.
USHIRIKIANO baina na Serikali ya
Wilaya ya Mufindi na Shirika la kuhudumia watoto SOS unatajwa kuimarsha uchumi
wa kundi la wanawake vijijini wakiwemo wajane waliokuwa wakikabiliwa na hali
duni ya kipato na kushindwa kuhudumia familia.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mufindi Robert Sungura alisema mradi wa uwezeshaji wanawake kiuchumi
umesaidia wanawake walio wengi kujiongezea kipato kwa kuanzisha shughuli za
ujasiriamali ikiwemo kilimo biashara
Miongoni mwa wanawake wa kikundi cha
akina mama Wajane cha kijiji cha Iyela wakizungumza wakati wa ukaguzi wa
shughuli za maendeleo ya vikundi wameeleza kuwa uwezeshwaji huo umewasaidia
kukidhi mahitaji ya familia.
Jumla ya Kaya 250 za wanawake wajane
zinazolea watoto wapatao 928 Wilayani Mufindi Mkoani Iringa walisema muda
mwingi walikuwa wakitaabika juu ya malezi ya watoto walioachiwa na wenzi wao
waliotangulia mbele za haki.
Wanawake hao walisema kuwa
wamefaidika na mradi uwezaji wanawake kiuchumi unao fadhiliwa na Shirika la
Kuhudumia watoto SOS Childrens Village Tanzania kwa Kilimo cha Nyanya na
Mahindi ambacho kimebadilisha maisha ya Akinamama hawa wa Kijiji cha Iyela
ambapo kimewafanya waweze kusomesha watoto,kujenga Nyumba na Kuongezeka kwa
Mazao kupitia elimu bora ya kilimo cha kisasa.
“Furaha ya wanawake hawa miongoni
mwao wakiwemo wajene ni juu ya mafanikio ya kiuchumi waliyoanza kuyapata
kutokana na mradi wa uwezeshwaji wanawake unaotekelezwa na shirika la Shirika
la kuhudumia watoto SOS kwa ushirikiano na Serikali ya wilaya ya Mufindi”
Wanawake hao waliongeza kuwa hapo
awali walikuwa wanapata kiasi cha gunia mbili za mahindi na kuwapelekea kwenda
kufanya kibarua sehemu nyingine lakini baada ya elimu iliyotolewa na Shirika la
Kuhudumia watoto SOS Childrens Village Tanzania imewaongezea kipato cha mazao
hadi kufikia kugunia kumi na saba.
Afisa Miradi wa Shirika hilo
anayesimamia Kilimo Doto
Solo alisema kuwa wanawake hao wajane walikuwa wamekata tamaa kutokana na ugumu
wa maisha wengi wao wakishindwa kuhudumia familia wakiamini kuwa hakuna njia
mbadala ya kujikoma kiuchumi hata jitihada za Shirika la SOS kwa kushirikiana
na serikali ya wilaya ya Mufindi zimefanikiwa kubadilisha mtazamo hasi
waliokuwa nao awali na sasa wamekuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake wengine.
Wengine
walikuwa na changamoto ya chakula kabisa wengine walikuwa wanahangaika kununua
na kutafuta msaada kwa wadau wengine hata ukiwaambia habari za vikundi na
shughuli za kiuchumi ilikuwa vigumu kuwaeleza ila mara baada ya kutoa elimu
sasa wamekuwa mfano kwa wanawake wengine.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Shirika La SOS Tanzania David Mlongo alitoa wito kwa
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kuongeza Kiwango cha Mikopo kwa Vikundi
vinavyofanya Vizuri katika Uzalishaji huku akiihimiza Halmashauri
kushirikiana zaidi kuwawezesha wanufaika hao kuanzisha kilimo cha kisasa kwa
kutumia nyumba kitalu
Mlongo
alisema kuwa mikopo hiyo itasaidia wanawake hao kuwekeza kwenye vitalu
nyuma kutokana na mikopo ambayo watakuwa
wamekopeshwa kwa kuwa kilimo cha aina hiyo kimekuwa na faida kubwa kuliko
kilimo cha kawaida kwa kuwa kilimo hicho hakina changamoto nyingi.
Lakini
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Robert Sungura aliwahimiza
wananchi wa wilaya ya Mufindi wakiwemo wa wanawake pamoja na vijana kutokata
tamaa katika suala la kujikwamua kiuchumi na badala yake waanzishe vikundi
vyenye lengo la kiuchumi na serikali iko tayari kuwawezesha kupitia mikopo
yenye masharti nafuu.
Shirika
hilo la SOS pia limewawezesha wanawake wa Kikundi cha Omaji kijiji cha Ukelemi
ambao wanajihusisha na Kilimo cha Umwagiliaji ambao kwasasa kipato chao
kimepanda kutokana na kuvuna mazao kwa wingi hususani Mahindi.
0 comments:
Post a Comment