Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi
wa Nangulukulu mkoani Lindi kuhusu ubovu wa barabara ya kutokea Lindi- Somanga
wakati alipokuwa akitokea Msibani Masasi mkoani Mwara leo tarehe 30 Julai 2020.
Wananchi wa Nangulukulu wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza
nao wakati akitokea Masasi leo.
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ukipita katika barabara ya Nangulukulu-hadi Somanga mkoani Lindi ambapo sehemu ya barabara yake imeharibika vibaya na kuhitaji matengenezo makubwa .
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na zawadi yake
ya Jogoo alilopewa na Shaweji Mohamed Kimbwembwe mkazi wa Somanga mkoani Lindi
ambaye alifurahishwa na utendaji kazi wa Mhe. Rais Magufuli wa kuwaletea
maendeleo Wananchi wanyonge.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Somanga Rehema Mikidadi
Ngenje Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa Shule hiyo ya Msingi ya
Somanga. Katika fedha hizo pia Rais aliagiza mwanafunzi huyo apewe Shilingi
laki moja kutoka kwenye fedha hizo mara baada ya kuibua kero ya Shule hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Wananchi wa
Somanga mkoani Lindi mara baada ya kuwahutubia wakati akitokea Masasi mkoani Mtwara.
PICHA NA IKULU.
0 comments:
Post a Comment