Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe akizungumza na
wamiliki wa viwanda vinavyozalisha saruji (pichani) kuhusu changamoto za bei ya
saruji katika maeneo mbalimbali nchini, mkutano huo ulifanyika katika Eneo huru
la Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje ya Nchi (EPZA), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe
akizungumza na wamiliki wa viwanda vinavyozalisha saruji (hawapo pichani)
kuhusu changamoto za bei ya saruji katika maeneo mbalimbali nchini, mkutano huo
ulifanyika katika Eneo huru la Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje ya Nchi (EPZA),
Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe, leo Julai 17, 2020
amekutana na wazalishaji wa Saruji nchini kujadili changamoto ya bei na
upatikanaji wa bidhaa hiyo ambapo amewataka kuongeza uzalishaji katika viwanda
vyao.
Akizungumza
Katika kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Eneo Huru la Uwekezaji kwa Mauzo
Nje ya Nchi (EPZA) Ubungo External jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu alisema kuwa sababu kubwa iliyofanya bidhaa
ya saruji kupanda bei ni pamoja na kuwepo kwa mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha
maeneo mbalimbali nchini.
“Katika
Mkutano huu changamoto zilizoelezwa na wazalishaji wa viwanda vya saruji nchini
ambapo imesababisha kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo ni pamoja na Mvua kubwa iliyokuwa
ikinyesha nchini nzima katika kipindi
cha mwezi Machi, Aprili na Mei ambapo iliathiri zaidi uzalishaji na
usafirishaji wa Saruji”, Alisema Prof.Shemdoe
Aidha,
Prof Shemdoe alisema kuwa changamoto ya mlipuko wa Ugonjwa wa Corona (COVID 19)
ambapo iliathiri uzalishaji kutokana na kukosekana kwa vipuli vya mitambo
inayotumika katika shughuli hiyo kwani huagizwa kutoka nje ya nchi.
Alibainisha
kuwepo kwa upungufu wa bidhaa hiyo kutokana na Serikali kutekeleza miradi
mikubwa inayoendelea nchini kama vile barabara za kisasa, ujenzi wa reli ya
kisasa (SGR), Ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha umeme (JNHPP) na ujenzi wa
hospital mbalimbali hapa nchini, pia ujenzi wa mji wa Serikali na Ikulu mpya ya
kisasa jijini Dodoma na ujenzi wa nyumba mpya za wakaazi jijini Dodoma.
Katika
kikao hicho Prof. Shemdoe ametoa rai kwa
wazalishaji wa Saruji kuongeza uwekezaji na uzalishaji katika bidhaa
hiyo ambapo kwa sasa ni muhimu kwa kuwa Serikali inatekeleza miradi mbalimbali
ambayo inahitaji saruji kwa wingi.
Aliongeza
kuwa wazalishaji kwa sasa wanapaswa kuangalia fursa katika ujenzi wa miradi
hiyo mikubwa na kujenga viwanda ili kuepusha gharama za usafirishaji wa saruji
kufika katika maeneo ya ujenzi wa miradi, pia aliwashukuru kwa kuitikia wito wa Serikali na kujadili hatma
ya kuondoa kero ya kupanda kwa gharama na upatikanaji wa Saruji.
“Kikao
hiki kimetoa mwongozo mzuri wa mwendelezo wa ushirikiano baina ya wawekezaji na
Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali kwani kitendo cha wenye Viwanda
kuridhia kwa pamoja kuongeza uzalishaji kufikia kiwango kilichokuwa awali pia
kutokupandisha bei kitasaidia bei kushuka na Saruji kupatikana kwa wingi ndani
ya muda mfup”, Alisema Prof.Shemdoe.
Nao
Wawekezaji na Wazalishaji Saruji nchini
wamepongeza hatua hiyo iliyochukuliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwani
imekuwa muhimili wa kuwaweka pamoja kuwasikiliza na kutatua changamoto
wanazokabiliana nazo na wamesema wapo tayari kushirikiana na Serikali katika
kuboresha uchumi wa Nchi na Maisha ya Watanzania.
0 comments:
Post a Comment