METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, July 9, 2020

NAIBU WAZIRI AKAGUA UJENZI WA VITUO VYA KUPOZA UMEME KATAVI NA TABORA

Mafundi wakindelea na ujenzi wa cha kituo cha Kupoza umeme cha Inyonga, kilichopo Wilaya ya Mlele,Mkoani Katavi,Julai,8,2020.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,(katikati) akikagua ujenzi wa kituo cha Kupoza umeme cha Ipole, kilichopo Wilaya ya Sikonge,Mkoani Tabora,Julai,8,2020.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Julai 8,2020  amefanya ziara ya ukaguzi wa  ujenzi ya vituo vya kupoza umeme(substation) vilivyopo katika Mkoani Katavi na Tabora.
Katika ziara yake hiyo, ya Ukaguzi wa Mradi wa njia kuu ya kusafirisha umeme wa Gridi ya Taifa kutoka Ipole Tabora hadi Mpanda Katavi,alikagua kituo cha Inyonga kilichopo mkoani Katavi na kituo cha Ipole kilichopo mkoani Tabora.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo,amesema ameridhishwa na kasi ujenzi ya mradi huo ambao unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu, mradi ambao unatarajiwa kuazalisha takribani megawati 28 za awali.
Aidha, amewataka wakandarasi wa mradi huo kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha mradi huo unamalizika kwa wakati ili kufanikisha lengo la mikoa hiyo  kuanza kutumia umeme wa Gridi ya Taifa.
“Mradi huu wa kupeleka umeme wa gridi ya Taifa katika mkoa wa Katavi ni miongoni mwa kipaumbele chetu kwakweli tutaendelea kusimamia mradi huu ili umalizike kama ulivyopangwa,”alisema.
Pia, amesema amefurahishwa kwa kupungua kwa gharama za ujenzi wa mradi ambao hapo awali ulikuwa ugharimu kiasi cha shilingi bilioni 135  lakini kwasasa utagharimu shilingi bilioni 70.
Vilevile,amelipongeza Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kwa usimamizi mzuri, na kuwataka kuendelea kwa usimamizi wa  ujenzi wa line ya kusafirishia umeme katika mradi huo, na  kuwataka kuendelea kutenga fedha kwaajili  ya ujenzi huo ili ukamilike kwa haraka.
Kwa upande wake, Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Neema Mushi amesema,mara baada ya kupewa maagizo ya kupeleka umeme wa gridi katika katika mkoa huo walianza  kazi hiyo mara moja ili kufanikisha lengo hilo,ambapo hadi sasa vituo vyote vipo katika hatua ya ujenzi ambao unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.
Pia, alisema mradi huo utakapomalizika utazalisha megawati 28 za awali ambapo kutakuwa na fida sita, ambazo mbili zitakuwa kwaajili ya matumizi ya viwanda na nne kwaajili ya matumizi ya wananchi.
Awali, akiwa mkoani Katavi, Naibu Waziri aliwasha umeme katika kijiji cha Nsekwa kilichopo, wilaya ya Mlele na kuwataka wananchi wa kijiji kutokuwa na wasiwasi kwasababu ujenzi wa kituo cha kuupoza umeme unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu na waakazi wa Katavi watapata umeme wa uhakika.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com