Muwezeshaji wa mafunzo kwenye upande wa sheria katika tansini ya habari akiendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa idara ya uandishi wa habari
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa idara ya uandishi wa habari wapigwa msasa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
WANAFUNZI wa chuo kikuu cha
Iringa idara ya uandishi wa habari wapigwa msasa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa
kuwaongezea upeo wa elimu ya uandishi wa habari katika Nyanja mbalimbali za
taaluma hiyo.
Akizungumza
wakati wa mafunzo hayo afisa wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika
(MISA) tawi la Tanzania Glory Kalinga alisema kuwa lengo la mafunzo hayo kwa ni
kuwaongezea uwezo wa kuitambua vizuri taalum hiyo ili wakihitimu masomo
wanatakiwa kwenda kutumia taalum hiyo kwa kufuata misingi na kanuni walizopewa
wakiwa chuoni.
Alisema
kuwa wanafunzi hao wanapaswa kuzijua sheria zilizopo katika sekta ya habari
ndio maana wakili yupo kwa ajili ya kutoa elimu ya kisheria na kuendana na
sayansi na teknolojia ambayo imekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara.
“Tunatoa
elimu hii kwa lengo la kuongeza uelewa na kwa wanafunzi hao wa vyuo vikuu ili
wakihitimu masomo yao waendelende wakafanya kazi ya uandishi kwa weredi
unaotakiwa kwa kuifanya tansinia hii kuwa imara na yenye wasomi wanaofata maandili,kanuni,sheria
na katiba ya nchi” alisema
Aliongeza kuwa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa
Afrika (MISA) tawi la Tanzania imekuwa ikitoa mafunzo ya mara kwa mara kwa
waandishi wa habari mbalimbali kwa lengo la nkumsaidia mwandishi wa habari
azitambue haki zake na kujitambua mwenyewe kwenye kazi yake.
Lakini
Kalinga aliziomba tasisi na mashirika mengine kuendelea kutoa elimu kwa
waandishi wa habari ili kuendelea kuikuza taaluma hiyo ambavyo imekuwa muhimu
katika maisha ya wananchi wengi katika nyanja mbalimbali.
Baadhi
ya wanafunzi chuo cha Iringa kikuu cha Iringa idara ya uandishi wa
habari wamejifunza kwa namna gani
wanaweza kupambana na changamoto za tansinia ya habari kutokana naelimu ambayo
wamepata kwenye mafunzo hayo ambayo yanafanyika kwa siku tatu katika chuo
hicho.
Walisema
wanaendelea kujifunza misingi ya wanahabari ili kufanya kazi kwa weredi mkubwa
wenye kuzingatia misingi na sheria za taalum hiyo ambayo imekuwa na changamoto
nyingi.
0 comments:
Post a Comment