Timu ya soka ya Rajaa Fc ya Kariakoo jijini Dar es Salaam ikiwa kamili kukabiliana na timu yoyote ile
TIMU ya soka ya Rajaa
Fc ya Kariakoo jijini Dar es Salaam inayoshiriki mashindao mbalimbali ya soka
zinazondaliwa jijini Dar es Salaam na nje imejipanga kufanya vyema katika
mashindano yoyote ikiwemo ligi ya kutafuta bingwa wa mkoa wa Dar es salaama
katika kuelekea madaraja ya juu zaidi nchini.
Wakizungumza na waandishi
wa habari,Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kassim Ramadhani na viongozi wake Mohamed
Abri walisema kuwa mara baada ya serikali kutangaza baadhi ya michezo kuendelea
kama kawaida timu hiyo iko katika mazoezi makali yanayofanyika katika viwanja
vya JK na Uhuru taifa kujiwinda na mashindano yoyote yatakayojitokeza
jijini Dar es Salaam.
Kocha Ramadhani
alisema kuwa wamejipanga katika suala zima la mazoezi kwani changamoto ilikuwa
ni gonjwa la Covid 19 ila kwa sasa tumeanza mazoezi makali kwani wachezaji
wengi walikuwa tu majumbani huku baadhi wakifanya mazoezi binafsi tofauti na
timu hivvo kwa sasa ni mazoezi mwanzo mwisho.
Alisema kuwa timu hiyo
imekuwa timu mojawapo ndogo zenye uongozi uliojipanga vyema kuhakikisha
inafanya vizuri kwenye ligi mbalimbali zinazoandaliwa jijini hapa kwa lengo la
kujiweka vyema na kuanza maandalizi ya kutafuta bingwa wa mikoa inayotarajiwa
kuanza wakati wowote.
Alisema kuwa wachezaji
wa timu hiyo wamekuwa katika hali nzuri na ni vijana wenye nia ya kufanya
vyema zaidi katika soka la Tanzania nje hivyo kuwa na njaa ya mafanikio chini
ya uongozi bora kabisa wa Mkurugenzi wa timu Mohamed Abri na nahodha wake
Salim Salehe Abri.
Aliongeza kuwa timu
hiyo imekuwa ikishiriki mechi mbalimbali za ndani ya jiji na nje ya jiji ambapo
walicheza mechi na timu ya Ligi Kuu ya Lipuli Fc mkoani Iringa na kuleta
upinzani mkubwa hali ambayo iliwapa nguvu ya kuweza kufanya vyema katika
mashindano yoyote watakayoshiriki.
Kwa upande wake,
Nahodha wa timu hiyo, Salim Salehe Abri alisema kuwa Klabu hiyo yenye wachezaji
vijana na wenye hali wako tayari kwa mashindano yoyote watakayoshirki kwani
wachezaji wako katika hali nzuri na kuwa na kila kitu ambacho wanahitaji kwa
sasa ikiwemo vifaa na jezi za uhakika kushiriki mashindano mbalimbali.
Abri aliwataka
wachezaji wa timu hiyo kufanya mazoezi kwa moyo kwa lengo la kuiletea mafanikio
timu biyo na kufanikisha malengo waliyojiwekea ya kuchukua ubingwa kwa kila
mashindano watakayoshiriki jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa kwa sasa
timu hiyo kwa kushirikiana na uongozi na wachezaji wameweka mikakati ya kufanya
vyema nchini kwa ujumla hali ambayo inatokana na ushirikiano mzuri
na viongozi wa timu na wachezaji pamoja na mashabiki wanaowaunga mkono
popote wanapokwenda
Abri ambaye ameshiriki
ligi mbalimbali za soka nchini amekuwa mstari wa mbele katika kuwapa moyo
wachezaji chipukizi wa timu hiyo kuweza kuonyesha zaidi vipaji kwa lengo
kujiuza zaidi katika ligi mbalimbali duniani kwa kupitia timu ya Rajaa
yenye mlengo wa kukuza vipaji za vya soka zaidi.
0 comments:
Post a Comment