Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma
na Utawala Bora wa Zanzibari, Mhe.Haroun Ali Suleiman (wa kwanza kulia),
akizungumza katika Kikao kifupi na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala B ora
walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Unguja, Zanzibari Juni 4, 2020, kulia ni
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu, Makamu Mwenyekiti Mohamedi
Khamis Hamadi, na kushoto ni watendaji kutoka Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma
na Utawala Bora wa Zanzibari, Mhe.Haroun Ali Suleiman, akizungumza na ujumbe
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Unguja, Zanzibari Juni 4, 2020,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibari,
Mhe.Haroun Ali Suleiman akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, na watendaji kutoka Wizara
yake mara baada ya mazungumzo mafupi kuhusu masuala ya haki za binadamu na
utawala bora,ujumbe huo ulimtebelea
ofisini kwake Mjini Unguja Zanzibari Juni 4, 2020.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibari, Mhe.Haroun Ali
Suleiman amesema kuwa Serikali inatakeleza jukumu kubwa la kuwapatia wananchi
huduma mbalimbali na kukidhi tafsiri halisi ya utawala bora katika kutekeleza
kazi zake.
Akizungumza
Ofisini kwake Mjini Unguja, Zanzibari alipotembelewa na ujumbe wa Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora amesema kuwa moja ya ishara ya utawala bora katika
nchi yeyote duniani ni pamoja na kuheshimu haki za binadamu kwa sababu ni
msingi mkubwa katika kutekeleza majukumu ya Serikali kwa kila mwananchi.
“Haki za
binadamu limekuwa ni jambo lenye mjadala kila kona kwa sababu kila jambo
linalotendeka liwe zuri au baya ni haki za binadamu, hasahasa jambo likiwa baya
utaambiwa umevunja haki za binadamu, Serikali yetu inatimiza jukumu kubwa la
kulinda haki za binadamu kwa kila mwananchi na huo ndiyo utawala bora”, Alisema
Waziri Suleiman
Alisema
kuwa katika utawala bora Serikali imejenga nidhamu kubwa ya kazi kwa watumishi
wote wa umma na imetenga siku ya utawala bora ambayo imeingizwa kwenye siku ya
maadili na hapa Serikali inajitathmini kwa mwaka mmoja kipi ambacho imefanikiwa
na kipi ambacho hajafanikiwa.
Aidha,
Waziri alisema kuwa katika utekelezaji wamasuala ya Utawala bora kwasasa hali
ni tofauti na zamani kwani kila mwananchi anapatiwa huduma ya haki kwa kutumia
kitengo cha Idara ya Msaada wa Sheria kilichopo Wizara ya Sheria na Katiba
ambacho kimekuwa msaada mkubwa kwa kila mwananchi wa Zanzibari.
“Mambo ya
utawala bora hapa Zanzibari yalianza zamani wakati wa Rais wa Kwanza wa
Zanzibari Hayati Abeid Karume alipoanzisha
Wizara ya kuweka hali za wananchi sawa nah ii ilikuwa na madhumi makubwa
kwani ilizingatia haki za binadamu kwa upana zaidi”, alisema Waziri Suleiman
Alibainisha
kuwa Tume ina jukumu kubwa la kusimamia haki za binadamu kwa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususani kusimamia tafsiri halisi ya neno haki
za binadamu, aliongeza kuwa kwenye
utawala bora Serikali yetu ya Tanzania umetimiza kwa kiasi kikubwa hasa kuleta
maendeleo Makubwa na nidhamu kazini.
0 comments:
Post a Comment