Mke wa Rais wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete kulia akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo vitabu viwili ambavyo vina taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi (CCM) kuanzia kipindi cha mwaka 2015/2020.
Mke wa Rais wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete ambaye pia alikuwa Mbunge wa kuteuliwa kupitia Mkoa wa Pwani na Lindi amesema ataendelea kushirikiana bega kwa bega na serikali katika miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ile ya kimikakati pamoja na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili wananchi.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa halfa fupi ya kukabidhi taarifa mbili za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi (CCM) pamoja na kitabu cha maswali na majibu aliyoyauliza wakati akiwa bungeni kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambapo ilihudhuliwa na wakuu wa mbali mbali wa idara ambapo amebainisha kazi mbali mbali ambazo amezitekeleza katika jamii katika kipindi chake cha miaka mitatu ikiwemo katika sekta ya afya, elimu,nishati ya umeme pamoja na kutatua changamoto za wananchi.
Aidha katika hatua nyingine Mama Salma Kikwete amepongeza Rais wa wamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kuweza kumteuwa kuwa Mbunge wa Bunge la Muungano wa Tanzania mnamo mwaka 2017 ambapo amedai kwamba kwake ni moja ya heshima kubwa ambayo imeweza kumpa fursa katika utekeleza wa Ilani ya chama cha mapinduzi pamoja na kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta mbali mbali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amempongeza Mama Salma Kikwete kwa kuweza kushirikiana bega kwa began a serikali ya awamu ya tano katika kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi pamoja na kushiriki kikamilifu katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo na miradi mbali mbali ya kimikakati.
0 comments:
Post a Comment