Na Agnes Geofrey
Waziri wa Madini mh Dotto biteko amepokea Madini yenye kilo 14 kutoka kwa mchimbaji mdogo wa Madini ya Tanzanite bw Saniniu Laizer Kurian ili kuuzwa kwa serikali.
Hafla hiyo iliyofanyika katika eneo la mererani mji mdogo wa Simanjiro mkoani manyara nakuudhuriwa na watendaji kutoka wizara ya Madini ,tume yamadini wadau wa sekta yamadini ,Naibu Waziri wa Madini ,Naibu Waziri wa Fedha na mipango ,wakuu wamikoa ya Kilimanjaro na manyara pamoja na wadau wote katika sekta yamadini.
Waziri wa madhini Mh Dotto Biteko alikabidhi kwa Naibu Waziri wa Fedha na mipango dr Ashatu kijaji, kama mlipaji mkuu wa serikali na hatimaye kukabidhiwa kwa Gavana wa banki kuu ya Tanzania profesa Florence Luoga nakuweka makubaliano ya utiaji wa sahini za hati za makabidhiano kisheria.
Waziri biteko amesema tukio hilo kwa mara yakwanza halijawai kutokea Tanzania kwan katika miaka ya nyuma uzalishaji wamadini hayo yalikuwa yakizalishwa licha ya uwepo wa utoroshwaji nakuisabababishia hasara serikali ,nakueleza kwasasa takwimu inaonyesha mapato yanayotokana na Madini nizaidi ya bilioni 520 sawa na Asilimia 111%
Akizungumza kwa Njia yasimu Mheshimiwa Rais wa Jamhuri yamuungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli kwanza amempongeza Mchimbaji huyo bw Saniniu Kurian Laizer Kuryani kwakukufanya uzalishaji mkubwa usio nakifani nakuiletea Nchi Maendeleo,licha ya Kutaka Madini Hayo kununuliwa na Serikali kwa Shilingi Bilioni 7 na milioni 700 uku dhamira ya mh Rais ni kuwekwa katika Makumbusho ya Taifa kwavizazi vijavyo ilikuwa kumbukumbu.
Hata hivyo awali Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mh Jems Olemilya
Alieleza kilio kikubwa kwa wachimbaji ni uwepo wa changamoto ya mitaji pamoja na vitendeakazi uku vile vilivyopo kuuuzwa kwa bei kubwa nakuumiza wachimbaji jambo ambalo ameiomba Banki kuu kukaa na Mataasisi yakifedha ili kuona namna wachimbaji wadogo kukopesheka.
0 comments:
Post a Comment