![]() |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza aliyesimama akifafanua jambo. |
Mkuu wa mkoa wa iringa amina masenza amesema hali ya amani katika mkoa wa iringa ipo shwari hivyo wagombea na wakeleketwa wa vyama mbalimbali ambavyo vinaona havijatendewa haki katika uchaguzi uliomalizika vinapaswa kupeleka malalamiko yao mahakamani na si kuandamana ili kupelekea uvunjifu wa amani ya mkoa huu.
Aidha ametoa shukrani zake kwa wadau na mashirika mbalimbali yakiserikali na yasiyo ya kiserikali kwa kutoa elimu ya uzalendo na pia madhehebu ya dini.
Pia mkuu huyo amesema amani haina Itikadi,Haijui kabila,madhehebu,kwani ikitoweka kuirudisha ni vigumu mno na huhitaji gharama kubwa-Maisha ya binadamu,fedha,mali na kadharika.
"Amani hii ikitoweka inaweza isirudi ikapelekea maisha ya mahangaiko miaka mingi kila mmoja wetu anawajibu wa kulinda amani iliyopo" Alisema masenza.
0 comments:
Post a Comment