Muongozaji wa majadiliano Bw. Michael Gwimile
akifafanua jambo wakati wa mkutano wa majadiliano uliowashirikisha wadau
mbalimbali wa Habari ulioandaliwa na MISA-Tan na kufanyika hivi karibuni Jijini
Dodoma
Muongozaji wa majadiliano Mrakibu Msaidizi wa
Polisi Bw. Athumani Mtasha akifafanua
kuhusu nafasi ya polisi katika kudhibiti makosa ya kimtandao na ushirikiano na
vyombo vya Habari wakati wa mkutano wa majadiliano ulioandaliwa na MISA-Tan na
kufanyika jijini Dodoma.
Washiriki
wa mkutano wa majadiliano wakiwa wamekaa kwa kuzingatia umbali wa mita moja
wakifatilia majadiliano wakati wa mkutano wa wadau kuhusu changamoto za
matumizi sahihi ya matumizi ya mitandao ya kijamii.
NA FREDY
MGUNDA, DODOMA
WATANZANIA
wametakiwa kutoa taarifa za uhakika katika mitandao ya kijamii ili kuondoa
upotoshaji ambao umekuwa ukiongezeka kila kukicha na kuzua taaruki kwa wananchi
na serikali kwa ujumla.
akizungumza na Waandishi wa Habari katika
warsha ya Taasisi ya Vyombo vya Habari kusini mwa Afrika kwa hapa nchini
Tanzania (MISA -TAN) iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa
Habari kwa lengo la kuwajengea Uwezo namna ya kuripoti Habari za COVID-19 bila
kuleta taharuki katika Jamii, Msemaji Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mrakibu Msaidizi Athuman Mtasha alisema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakisambaza taarifa
za mamlaka mbalimbali zisizo wahusu bila uchunguzi matokeo yake husababisha
uchochezi ,takwimu za uongo na kusababisha taharuki katika jamii hivyo ni vyema
watu wakaacha mara moja tabia ya kusambaza taarifa kwani zinaweza kuwatia
hatiani.
Alisema kuwa Kwa
mujibu wa takwimu za mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kumekuwa na
ongezeko kubwa la Matumizi ya mitandao ya kijamii nchini Tanzania na ongezeko
hilo limepanua wigo wa utoaji na upatikanaji wa taarifa miongoni
mwa Wananchi na Taasisi mbalimbali.
Mtasha
alisema kuwa mitandao ya kijamii hususani facebook, twitter, Instagram na
youtube imewawezesha wananchi kuzalisha, kusambaza na kupata taarifa mbalimbali
za matukio yanayojiri katika jamii kwa haraka Zaidi kuliko redio, televisheni na magazeti.
“Pamoja
na fursa hii kumekuwa na changamoto ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii
zikiwemo upotoshaji, udhalilishaji na matumizi mengine yasiyofaa na Hii
inajidhihirisha kwenye kuongezeka kwa kesi za makosa ya kimtandao katika miezi
ya hivi karibuni” alisema
Afisa sheria Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
[TCRA]Kanda ya kati Joseph Kavishe amesema mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa
kushirikiana na vyombo vingine likiwemo Jeshi la polisi imeendelea
kusimamia kwa ueledi vyombo vya Habari Pamoja na watumiaji wengine wa mitandao
.
“TCRA imeendelea kusimamia
kwa ukaribu sana vyombo vya Habari Pamoja na watumiaji wengine wa mitandao, kwa
Maagizo ya Mhe.Rais kuhusu taarifa za Uzushi yeyote anayekamatwa lazima taraibu
za kisheria kufuatwa,TCRA inasimamia vyombo vya Habari kwa mashauriano pengine
panapokuwa na changamoto Fulani ya utoaji wa Habari huwa kuna kamati ya
maudhui na si kila kosa lazima kuadhibiwa na makosa mengine kamati ya maudhui
hukaa na kuwaonya wahusika ili kuacha kuleta mkanganyiko katika jamii”amesema.
Mjumbe wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini
mwa Afrika Michael John Gumile ambaye pia ni Mhadhili kutoka chuo Kikuu
cha Mtakatifu Yohana (St.John) alisema
Warsha hiyo ya
wanahabari imesaidia wadau wa Habari namna ya kuandika Habari zitakazosaidia
kuondoa taharuki katika jamii hususan katika kipindi hiki cha Corona.
“Sasa hivi nchini na Dunia kwa ujumla hivyo wadau wa Habari
tumekutana hapa katika kujenga msingi mzuri ili kuhakikisha taarifa sahihi
zinapatikana na watu kuzifanyia maamuzi na taarifa ambazo haziwezi kuleta
mkanganyiko katika jamii”amesema.
Meneja wa kituo cha
Redio,Dodoma FM ,Zania Miraji ni miongoni mwa wadau wa Habari waliohudhuria
katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini
Mwa Afrika ,hapa nchini(MISA-TAN) alisema warsha hiyo imekuwa mwarobaini wa
kuwakumbusha waliojifunza kutoka vyuoni na na maelekezo yaliyotolewa katika
warsha hiyo watayafanyia kazi hususan namna ya kuandika Habari ambazo hazina
mkanganyiko pia namna ya mwanahabari ya kujikinga
0 comments:
Post a Comment