METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, May 22, 2020

NI WAJIBU WA KILA MFANYAKAZI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE IAPASAVYO-MHANDISI KANGOLE

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mhandisi Eustance Kangole akisisitiza jambo wakati akifunga mkutano wa Baraza la wafanyakazi  kilichofanyika kwa siku mbili tarehe 21-22 Mei 2020 Jijini Dodoma katika ukumbi wa Chuo cha Ujenzi mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mhandisi Eustance Kangole akisisitiza jambo wakati akifunga mkutano wa Baraza la wafanyakazi  kilichofanyika kwa siku mbili tarehe 21-22 Mei 2020 Jijini Dodoma katika ukumbi wa Chuo cha Ujenzi mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mhandisi Eustance Kangole akisisitiza jambo wakati akifunga mkutano wa Baraza la wafanyakazi  kilichofanyika kwa siku mbili tarehe 21-22 Mei 2020 katika ukumbi wa Chuo cha Ujenzi mkoani Morogoro. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TUGHE NFRA Makao Makuu Mathias Mganga (Kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa (Kulia).

Na Mathias Canal, NFRA-Morogoro

Wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wametakiwa kutimiza wajibu wao katika kutekeleza malengo waliyopangiwa.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mhandisi Eustance Kangole wakati akifunga kikao hicho kilichofanyika kwa siku mbili tarehe 21-22 Mei 2020 Jijini Dodoma katika ukumbi wa Chuo cha Ujenzi mkoani Morogoro.

Mhandisi Kangole amesema kuwa matakwa ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kwa dhati kuboresha maslahi ya wafanyakazi hivyo ili kufikia adhma hiyo ni wajibu wa kila mfanyakazi kutekeleza wajibu wake ipasavyo.

Kadhalika amesisitiza ulazima wa kutekeleza kwa kina Mipango na malengo yaliyoanishwa kwa mujibu wa taratibu za kisheria lakini pia mipango mbalimbali iliyoainishwa.

Mhandisi Kangole amewaasa wafanyakazi wote kutekeleza majukumu kwa kuzingatia Uadilifu, kujituma, ufanisi, weledi na maarifa ili kutimiza adhma ya serikali.

Kadhalika ameitaka Menejimenti ya NFRA kuzingatia maslahi ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi yao ili waweze kufanya kazi kwa bidii.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com