Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza na
waandishi wa habari hawapo pichani Jijini Dar es Salaam, kuhusu kurejeshwa kwa
huduma za utalii nchini, kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB, Bi. Devota
Madachi.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii (TTB), Bi. Devota Madachi akiandika
swali kutoka kwa waandishi wa habari katika Mkutano wa Waandishi wa habari na
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo pichani Jijini Dar es
Salaam, kuhusu kurejeshwa kwa huduma za utalii nchini.
Hayo yamesemwa leo Jumatano (Mei 20, 2020) Jijini Dar es
Saalam na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Jaji mstaafu Thomas Mihayo wakati wa mkutano
wake na Waandishi wa Vyombo vya Habari
kuelezea mikakati endelevu ya TTB katika kutangaza shughuli za utalii nchini.
Jaji Mihayo alisema kufuatia kikao baina ya wadau wa utalii
na Serikali kilichofanyika hivi karibuni Jijini Arusha, Wizara ya Maliasili na
Utalii imeandaa mwongozo mahsusi wa namna ya uendeshaji wa shughuli za utalii
nchini na unaotarajiwa kutafsiriwa kwa lugha mbalimbali na kusambazwa katika
masoko ya utalii sehemu mbalimbali duniani.
‘Bodi ya Utalii Tanzania imeshiriki kikamilifu kwenye kikao
hicho na mwongozo uliotolewa
utahakikisha kuwa Watanzania wanakua salama na watalii pia wanatalii kwenye vivutio
vilivyo na usalama na kuhakikisha kuwa shughuli za kutangaza utalii hazisimami
kutokana na janga la corona duniani’’ alisema Jaji Mihayo.
Kwa mujibu wa Jaji Mihayo alisema TTB pia imepanga kufanya
kufanya ukaguzi wa maeneo mbalimbali ya kupokelea na kulaza watalii ili
kujiridhisha kuwa maeneo hayo yana huduma mbalimbali za dharura kulingana na
mwongozo ulitolewa na Serikali ili kuhakikisha kuwa utalii wa Tanzania
unaendelea kuwa salama.
Aidha Jaji Mihayo alisema mara baada ya zoezi hilo
kukamilika TTB itaanza kufanya mazungumzo na Ofisi za Ubalozi wa Tanzania na
Balozi za masoko ya utalii wa Tanzania zilizopo nchini ili kuwahakikishia hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusiana
na udhibiti wa mlipuko wa virusi vya COVID-19 kabla ya kuruhusu watalii kuanza
kuwasili nchini.
Akifafanua zaidi Jaji Mihayo alisema TTB kwa kushirikiana na
sekta binafsi imetengeneza filamu mbalimbali za vivutio vya utalii nchini ili
kuhakikisha kuwa shughuli za kutangaza utalii hazisimami kutokana na janga la
CORONA, ikiwemo kampuni ya Great Migration Camp walioanzisha kipindi cha ‘Serengeti Live Show’ kinachorushwa
katika mitandao yote ya kijamii ya TTB na Serengeti
Live YouTube Channel.
‘Nitoe wito kwa wafanyabiashara wa sekta ya utalii,
kujitolea kwa hali na mali kutangza filamu hizi ambazo zimesaidia kutangaza
utalii wa Tanzania duniani, na televisheni zetu za ndani zinaweza kuzipata
filamu hizi bure bila malipo hapa TTB ili mkaziongeze kwenye ratiba za vipindi
vyenu kama sehemu ya kutoa elimu’ alisema Jaji Mihayo.
Kwa upande Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB, Devota Mdachi
alisema mwishoni mwa mwezi huu, ndege ya kwanza inatarajia kutua nchini ikiwa
na watalii ambapo hadi sasa tayari wadau wote wa utalii wamekamilisha miongozo
mbalimbali inayotakiwa kufuatwa ili kuwakinga watalii na maambukizi ya virusi
vya COVID-19.
Aidha Mdachi alisema Serikali pia i imefanya mawasiliano na
Ofisi za Ubalozi wa Tanzania katika nchi za Israel, China na Malaysia ili
kuhamasisha makundi makubwa ya watalii
wa nchi hizo waliopanga kuja Tanzania mwanzoni mwa mwaka huu kufufua mipango
yao ya safari ya kutembelea vivutio vya utalii nchini.
Aidha Mdachi alisema kwa kuzingatia mwongozo uliopo Serikali
tayari imeanza kufanya mazungumzo na makampuni za uwakala wa utalii katika nchi
India, Malaysia na Israel.
0 comments:
Post a Comment