Makatibu Wakuu wakitaza kazi ya ujenzi ghala la kuhifadhia mazao kijiji cha Mbogo Komtongo wilaya ya Mvomelo ambalo muda wake wa ujenzi umeisha lakini halijakamilika.Wa kwanza toka kushoto ni Bw.Gerald Kusaya (Wizara ya Kilimo),Bw.Gerald Mweli(Naibu Katibu Mkuu,OR-Tamisemi na Prof.Riziki Shemdoe ( Katibu Mkuu Viwanda na Biashara) na wa wa kwana kulia ni Mratibu wa Mradi wa ERPP Eng.January Kayumbe
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (aliyeshika kofia) akiwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Balozi Joseph Sokoine wakikagua mradi wa ujenzi ghala la kuhifadhia mpunga kijiji cha Kigugu wilaya ya Mvomelo jana
Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akiongoza kamati ya makatibu wakuu kukagua skimu ya umwagiliaji zao la mpunga katika kijiji cha Mvumi wilaya ya Kilosa jana.Uzalishaji katika skimu hiyo umeoanda toka tani 2.5 kwa ekari hadi tani 5.5 za mpunga kwa ekari.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya
ametoa onyo kali kwa wakandarasi waliozembea kukamilisha miradi ya ujenzi wa
miundombinu ya skimu za umwagiliaji wilaya ya Mvomero na Kilosa
Kusaya ametoa onyo hilo jana (22.04.2020)
wakati alipoongoza ziara ya wajumbe wa kamati ya tendaji ya utekelezaji wa
Mradi wa Kuongeza Thamani zao la mpunga ( Extending Rice Production
Project-ERPP) katika mkoa wa Morogoro
Makatibu Wakuu wengine walioshiriki ziara hiyo
ni Prof.Riziki Shemdoe (Viwanda na Biashara) pia Naibu Katibu Mkuu Balozi
Joseph Sokoine (Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira) na Naibu Katibu Mkuu Gerald
Mweli (Ofisi ya Rais-Tamisemi)
“ Hatujaridhishwa kabisa na wakandarasi wa
ujenzi wa maghala ya kuhifadhia nafaka ya kijiji cha MbogomKomtonga na Kigugu
kwa kutokamilisha kazi ndani ya mkataba ” alisema Kusaya kwa niaba ya kamati
hiyo.
Katika hali isiyo ya kawaida kamati ya Makatibu
Wakuu ilichukizwa na kitendo cha mkandarasi
M/s AMI & VAI Investment ya Dar es Salaam anayejenga ghala la
kuhifadhia mpunga kijiji cha Kigugu wilaya ya Mvomelo kwa gharama ya shilingi
Milioni 816.37 alikimbia eneo la mradi
licha ya kuwa na taarifa za ujio wa makatibu wakuu.
Alipoulizwa alipo mkandarasi wa mradi
huo,msimamizi wa mafundi Abdul Kabanika
alisema “ Bosi tulikuwa naye hapa muda mfupi uliopita lakini sasa
hatumuoni .”
Taarifa zilisema kampuni hiyo ya M/s Ami
&Vai Investment imeshindwa kumaliza kazi ndani ya mkataba ulioisha tarehe
21 Aprili 2020 na ujenzi upo asilimia 70 .
“Natoa muda hadi ifikiapo saa 11 jioni leo
(Jumatano) mkandarasi M/s AMI & VAI
Investment awe amejisalimisha kwangu,kwani ajue serikali ina mkono
mrefu.Tutamsaka kotote na kumrejesha hapa Kigugu atueleze kwanini kazi yetu
hajakamilisha” alisema Kusaya.
Kamati ilikagua pia mradi wa ghala kijiji cha
Mbogo Komtongo ambao ujenzi wake umefikia asilimia 70 chini ya mkandarasi M/s Shekemu kwa gharama ya Shilingi Milioni
790.87 lakini haujakamilika.
Katibu Mkuu Kusaya alionya na kusema
kutokamilika kwa miradi hii kutakua ni kikwazo kwa wakulima kukosa mahala pa
kuhifadhi mazao yao na lengo la serikali kutotimia.
Awali kamati hiyo ilitembelea skimu ya
umwagiliaji kijiji cha Mvumi wilaya ya Kilosa na kujionea hali ya miundombinu
kwa ajili ya mashamba ya mpunga ya wakulima iliyofikia asilimia 84 ya ujenzi
mitaro na banio.
Skimu hiyo inajengwa kwa gharama ya shilingi
Bilioni 1.97 na mkandarasi M/s Whitecity International Ltd akishirikiana na M/s
Skyline Properties Ltd na kwa mujibu wa mratibu wa mradi kiasi cha shilingi
Milioni 713.15 zimelipwa sawa na asilimia 54.
Alipoulizwa kwanini mradi haujakamilika
msimamizi wa mradi huo Mhandisi Emanuel Norbet alisema wamechelewa kukamilisha
kutokana na uwepo wa mvua nyingi msimu huu zilizoharibu miundombinu ya barabara
na mitaro.
Katika hatua nyingine ,kamati iliridhishwa na
kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao kijiji cha Mvumi
wilaya ya Kilosa kwa asilimia 99 lililojengwa na mkandarasi M/s B.H Ladwa Ltd
kwa gharama ya shilingi milioni 971.31 ambapo tayari shilingi milioni 536.06
zimelipwa.
Baada ya ukaguzi wa miradi hiyo Katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo alisema serikali itahakikisha sheria inachukuliwa ili mkradi
ikamilike kwa mujibu wa mikataba.
“Mikataba
yote imekwisha,nataka miradi hii iishe na wakulima wapate maji kwa ajili
ya kutekeleza kalenda zao za kilimo na serikali ya Rais John Magufuli haitaki
wakandarasi wazembe.Tunataka wakulima wapate maji kwenye mitaro ili waendelee
na kilimo cha mpunga” alisema Kusaya
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda
na Biashara Prof.Riziki Shemdoe amewaagiza washauri wasimamizi wa miradi hiyo
ambayo haijakamilika kuchukua sheria na kuanza kukata fedha kwa wakandarasi
wazembe.
“ Hatua za kisheria kukata fedha kwa mujibu wa
mkataba zichukuliwe haraka,kwani mikataba imeisha na muda wa nyongeza
umeisha.Fedha ya serikali ianze kukatwa kila siku (liqudated damages) “ alisema
Prof.Shemdoe
Akizungumza hatua alizochukua msimamizi wa
miradi ya ujenzi wa maghala Kigugu na Mbogo Komtonga Architect
Ismail Mvungi aliwajuisha wajumbe kuwa tayari wameanza kuwakata wakandarasi
hao kiasi cha shilingi 400,00 kila siku kwa kuchelewa kukamilisha kazi.
Mradi wa mradi wa ERPP Mhandisi January Kayumbe
alisema miradi hiyo ya ujenzi ilitekelezwa kwa mwaka mmoja na muda wake
unamalizika 30 Aprili 21 mwaka huu
,hivyo wakandarasi ambao hawajakamilisha taratibu za sheria zitafuatwa.
Akishukuru kwa niaba ya wananchi Mwenyekiti wa
Kijiji cha Kigugu kata ya Sungija wilaya ya Mvomelo Damas Mnyani alisema miradi
hii itasaidia kuongeza uhakika wa upatikanaji maji kwenye mashamba ya mpunga
hali itakayoongeza uhakika wa uzalishaji.
“ Kuwepo kwa skimu hizi kwenye vijiji vyetu
kutasaidia kuondoa tishio la njaa kwani tutalima mpunga mwaka mzima na
kuhifadhi kwenye maghala tuliyojengewa na serikali yetu.” Mnyani
Mradi huo umefanikiwa hadi sasa kuongeza
uzalishaji zao la mpunga toka tani 2.5 kwa ekari hadi tani 5.5 kwa ekari baada
ya miundombinu kuboreshwa.
Mradi wa ERPP ulianza kutekelezwa mwaka mwaka
2015 kwa gharama ya Dola za kimarekani milioni 22.91 toka Benki ya Dunia
ukijusisha Tanzania Bara na Zanzibar.
Jumla ya
miradi 11 ikiwemo ujenzi wa skimu 5 za umwagiliaji,ujenzi wa maghala 5 na
ujenzi wa maabara moja ya mbegu
inatekelezwa katika mkoa wa Morogoro chini ya ERPP.
0 comments:
Post a Comment