Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka (aliyesimama) akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ( aliyekaa kulia) wakati wa kikao cha wadau wa zao la pamba mjini Simiyu leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akinawa mikono kwa maji na dawa alipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuanza ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na wizara ya kilimo .
Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( aliyevaa tai) akitoa maelekezo kwa Maj.E. Buberwa msimamizi wa mradi wa ujenzi wa jengo la wizara ya Kilimo katika viwanja vya Nane nane Nyakabidi Bariadi mkoani Simiyu
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (aliyeshika dumu ) akitazama bidhaa za mafuta yanayozalishwa na kiwanda cha kuchambia pamba cha NGS Bariadi mkoa wa Simiyu leo
Wizara ya Kilimo imewataka wananchi wa Mkoa wa
Simiyu kuongeza uzalishaji wa zao la pamba sambamba na mazao mengine mengine ya
biashara ili kuwa na uhakika wa mapato
Kauli hii imetolewa leo mjini Bariadi na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya wakati aliopongea na wanunuzi wa zao la
pamba katika kikao kilichofanyika ofisini kwa Mkuu wa Simiyu.
Katibu Mkuu huyo amewasihi viongozi wa mkoa wa
Simiyu kuwahamisha wakulima pamoja na kuzalisha zao la pamba watumie ardhi
iliyopo kuzalisha zao la mkonge na korosho yanayoweza kustawi vizuri kwenye
mkoa huu.
“ Nawashawishi wakulima wa Simiyu pamoja na
kulima pamba kwa wingi pia walime mkonge pia kwani tunacho kituo chetu cha TARI
Mlingano chenye uwezo wa kuzalisha na kusambaza mbegu bora za mkonge hadi
hapa.” Alisisitiza Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Kusaya amesema anatambua uwepo wachangamoto
za madai ya baadhi ya wakulima wa zao la
pamba pamoja na halmashauri kutokana na ushuru kutolipwa na kuwa serikali
itafikia suluhu ya jambo hili.
Amewataka wanunuzi wa zao la pamba kuendelea na
maandalizi ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Mei na kuwa
serikali inaendelea kushughulikia madai hayo
Kusaya alisema ifike wakati kama kulikuwa na
makosa yalifanyika huko nyuma kuhusu msimu wa pamba sasa lazima tuangalie
wanunuzi na serikali tumejiandaa namna gani
“Ifike mahala kama kuna makosa tuliyafanya huko
nyuma yasiathiri uuzaji wa pamba ya wakulima kwani wana imani sana na serikali
ya Awamu ya Tano.Ndio maana nimetembelea mikoa hii ya Simiyu,Shinyanga na pia
nitaenda Mwanza kujionea hali ya maandalizi ya msimu wa pamba” Kusaya
Katika
kikao hicho Kusaya aliwaomba viongozi wa mkoa wa Simiyu na wa Chama cha
Mapinduzi kushirikiana wizara ya Kilimo kutengeneza mazingira mazuri ya
wakulima kuendelea kunufaika na kazi zaokwa kupata soko la uhakika .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony
Mtaka alisema mkoa wake ndio unaoongoza nchini kwa uzalishaji wa pamba na kuwa
wakulima wana imani na serikali katika kuhakikisha wanapata fedha zao
zilizosalia
Mtaka aliyataja kiasi cha Shilingi Bilioni 3.5
bado hakijalipwa kwa halmashauri za mkoa wake kama ushuru wa mazao kutoka kwa
wanunuzi na kiasi cha Shilingi Milioni 794 kinadaiwa na wakulima hadi sasa.
Mkoa wa Simiyu katika msimu wa mwaka 2018/2019
ulizalisha kilo milioni 166.19 za pamba na kuufanya ushike nafasi ya kwanza
kitaifa.
0 comments:
Post a Comment